MAKAMU
wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, amesema anawasahangaa
waumini wa dini mpya inayohamasisha na kuwashawishi waumini wa dini ya
kiislma na watanzania kugomea zoezi la kuhesabiwa Sensa na watu na
Makazi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana baada ya zoezi lamkusebiwa,
Maalim , alisema kuwa kuna watu wachahe tu ambao hawajulikani
walipoibukia ambao wanaamini kuwa wao ndiyo hasa wanaijua dini vilivyo
kuliko hata wazee wao.
Aidha
Maalim, aloiwataka wanavisiwani na watanzania wote kwa ujumla kuwapuuza
watu hao wanaoeneza ujumbe na kampeni ya kuvuruga zoezi hili la
kitaifa, na kuwataka kutoa ripoti kwa polisi haraka kwa atakayemgundua
mtu wa namna hiyo, ili achukuliwa hatua za kisheria haraka.
Akifafanua
zaidi, Maalim, alisema kuwa ''zoezi hili la Sensa wala si la kwanza
kufanyika nchini Tanzania, na wala halikuwahi kuwa na kipingamizi na pia
tangu enzi za mababu zetu na duniani kote hufanyika zoezi kama hili,
wala haijawahi kutojitokeza dini ya kupinga ikidaai si halali kidini,
jambo itu ambalo linashangaza sana''. alisema
UCHUNGUZI WA MAFOTO
Siku
za hivi karibuni kumekuwa kukiibuka makundi kadhaa yanayojiita
wanaharakani na wengine Uamsho, ambapo miongoni mwa wengi wanaounda
makundi hayo ni vijana na wazee wachache ambao nao kwa namna moja ama
nyingine ukifuatilia 'back ground' ya maisha yao ni wale walioishapitia
misuko suko fulani ya kimaisha.
Kwa
uchunguzi wa harakaharaka uliofanywa na mtandao huu, umegundua kuwa
wapo vijana wengi wenye umri usiozidi miaka 40, wakiongozwa na wazee
wachache kwa imani yao binafsi na wengi wao ni wale waliomrudia mungu
aidha kwa kushawishiwa ama kutubia baada ya kuwa jambo fulani ambalo
halimpendezi mungu kwa muda fulani.
Wengi
wao utakuwa ni wake ambao aidha siku za nyuma waliwahi kuwa wavuta
bangi na unga ama walevi wa kilevi chochote, ogopa sana mtu kama huyu
pindi anapogundua kuwa alikuwa akipotea na kuamua kumrudia mungu basi
kila kitu kwake yeye kitakuwa ni haramu kutokana na kwamba anakumbuka
yale aliyokuwa akiyafanya siku za nyuma.
Kwa upande wangu sihani kama Zoezi la kuhesabiwa Waislamu kuwa linatatizo lolote kidini, na wala halihusiani na imani za kidini.
Tarehe
25/8 2012 mida ya saa 10:50 jioni mtandao huu ulipokea Meseji
inayohamasisha kutoshiriki katika zoezi hilo, ambapo mwisho wa meseji
hiyo ilitakiwa iandikwe katika mtandao huu ili iweze kusomwa na watu ama
kuwatumia watu 10 na zaidi.
MESEJI HIYO ILIANDIKWA HIVI:- Yaa''
ALLAH'' natamka mimi ninaesoma SMS hii kwa kauli yangu na wewe
''ALLAH'' ukiwa shahidi, kwamba sito shiriki zoezi la SENSA mpaka
kipengele cha ''DINI'' kiwemo katika ''DODOSO'' za ''SENSA''.
Sitoshiriki maana huo ndio msimamo wa ''WAISLAMU'', na kama nitashiriki,
allah unajua nini malipo ya ''WANAFIKI'' Daima narudia tena sita
shiriki ''SENSA'', Ewe ALLAH shuhudia. Tuma SMS hii kwa watu kumi
kuashiria kwamba tuko pamoja tuseme hatuesabiwi SENSA. MWISHO WA KUNUKUU MESEJI HIYO.
''Hivi
mpaka unaacha kukaa na kufikilia maendeleo ya Familia yako na tanzania
kwa ujumla unakaa chini na kuanza kutunga SMS kama hii ambayo haina tija
kwako wala haitakungea lolote katika maisha yako unakuwa unafikilia
nini, na pia unapotoa agizo kwa uliyemtumia kuwa atume kwa watu kumi, je
umemtumia na vicha ya kufanya kazi hiyo?, Jamani tubadilike dunia ya
sasa tunakoelekea ni maisha ya Sayansi na Teknolojia na tunaelekea
Kidigital zaidi, tunatoka analogi, tusipoangalia Waislamu tutabaki na
majungu tu huku wenzetu wakisonga mbele maana kila kukicha wao
wanamiradi mipya na plani mpya sisi je tunanini????????? Haya ni mawazo yangu Wadau.
No comments:
Post a Comment