Mratibu wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy, akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu. (Picha zotena Executive Solutions)
Wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba wakitembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Mratibu wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy, akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba wakitembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Mshambuliaji hatari wa Simba, Mrisho Ngassa akisalimia wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Wechezaji wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Kocha
Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic akiongea na Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe kwenye hafla iliyofanyika
baada ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba kutembelea kiwanda cha
TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.
Wechezaji
wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na viongozii wa kiwanda
cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki
ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio
mdhamini wao mkuu.
Wechezaji
wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa
wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo
ndio mdhamini wao mkuu.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Timu
ya Simba Sports Club ambayo imeweka kambi mkoani Arusha imefanya
ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza bia cha TBL kilichopo
jijini hapa.
Akiongea
katika ziara hiyo mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa timu hiyo
Ibrahimu Masoud Maestro alisema kuwa wao kama timu ya Simba wameamua
kufanya ziara yao katika kiwanda hicho ili kuweza kujionea mambo
mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio wadhamini wakuu wa timu yao.
Alisema
kuwa Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa
katika mambo mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari
ya usafiri jezi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo hivyo
wamefurahishwa sana na jinsi walivyopokelewa vizuri kiwandani hapo na
aliwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
Akiongea
kwa niaba ya kampuni hiyo Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo hiki cha timu hii ya Simba
kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao na kuona kazi
ambazo zinafanywa na kampuni hii.
Alisema
kuwa TBL inathamini mchango wa timu za Simba na Yanga kwa soka la
Tanzania na ndio maana imekuwa ikizidhamini timu hizi kwa muda mrefu
huku akibainisha kuwa wataendelea kudhamini timu hizi hadi mwisho.
Alibainisha
kuwa timu hizi mbili zimekuwa zikifanya mambo makubwa kwani zimekuwa
zikiwapatia vijana mbalimbali ajira kwa kupitia timu zao.
Aliwasihi
wananchi kwa ujumla kuendelea kuisapoti timu hizi kwani ndio timu mbazo
zina wachezaji wengi zaidi wanaochezea timu ya taifa.
Kavishe
alisema kuwa kupitia kudhamini timu hizi pia wamekuwa wakijitangaza
sehemu mbalimbali kwani iwapo timu ikienda kucheza nje ya nchi wanaenda
kukitangaza kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager hivyo
wanafanya kampuni hii pamoja na bia ya Kilimanjaro kuwa juu zaidi.
No comments:
Post a Comment