Mchezaji wa Pool wa Klabu ya Jambo Lee, Michael Saita
akicheza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa
kwa awamu ya pili katika klabu ya Jambo
Lee Kawe jijini Dar es Salaam.Kulia ni mchezaji wa klabu hiyo Judith Machafuko.
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya Safari Pool Taifa yamefunguliwa tena jana kwa
awamu ya pili baada ya kusimama kwa mwezi mmoja kwa mfungo wa Ramadhani.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhazini wa Chama cha Pool
Taifa, Zaholo Ligalu alisemakatika awamu ya kwanza mikoa kumi tayari
imeshakamilisha mashindano hayo ya ngazi ya mikoa na mikoa sita ndio inakwenda
kuanza leo kumalizia awamu ya pili baada ya mfungo wa Ramadhani ambayo ni
Mbeya,Iringa,Dodoma, Temeke,Ilala na Kinondoni.
Ligalu alisema Kinondoni,Temeke na Ilala wanaanza leo ambapo
Mbeya ,Iringa na Dodoma wataanza Septemba 6 mwaka huu na kumaliza Septemba 9
mwaka huu.
Alisema Ligalu mashindano ya mwaka huu yanahusisha timu za vilabu kwa ngazi ya mikoa na fainali
za kitaifa ambazo zinatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 27,28,29 na 30 mwaka
huu ambapo klabu ambayo ni bingwa wa mkoa ndio atawakilisha Mkoa katika
mashindano hayo.
Zawadi ya mshindi wa kwanza kwa ngazi ya Mkoa upande wa timu
ni shilingi laki saba na kwa ngazi ya Taifa itakayofanyika mkoani Mwanza
mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni tano
No comments:
Post a Comment