NDG WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO ,
HIVI
KARIBUNI RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI TANZANIA [TFF] NDG
LEODGER CHILA TENGA ,ALINUKULIWA NA VYOMBO VYA HABARI KARIBU VYOTE
VILIVYOKO NCHINI TANZANIA ,AKITOWA MAELEKEZO KWAMBA SASA TFF IKO MBIONI
KUANZA KUWADHIBITI WACHEZA MPIRA WA MIGUU WA NCHI HII YA TANZANIA
WANAOTUMIA MADAWA YA KULEVYA HUSUSAN BANGI, GANJA, HASHISHI ,NA HATA
NDUMU- KAMA WATUMIAJI WENYEWE WANAVYOIPAMBA KWA MAJINA HAYO HUKO
MITAANI.
UAMUZI WA RAIS HUYU
MUADILIFU WA TFF UNAPASWA KUPONGEZWA NA VIONGOZI WA MICHEZO WOTE KATIKA
NCHI HII YA TANZANIA ,HASA KWA KUZINGATIA HATIMA YA WACHEZAJI WAVUTA
BANGI MARA WATAKAPOKUWA WAMEFILISIKA UWEZO WA VIWANGO VYAO ,NA
WATAKAPOKUWA NJE YA UWANJA KAMA WATAZAMAJI WA KAWAIDA .
NINAO USHAHIDI WA
KUTOSHA KWAMBA WAPO BAADHI YA WACHEZAJI WA ZAMANI NA WALIKUWA NI WAZURI
MNO AMBAO MPAKA HIVI SASA WAMEPOTEZA MUELEKEO BAADA YA KUWA NJE YA MPIRA
WA MIGUU NA WALIKUWA WAKIVUTA HIZO BANGI NA SASA WAMEKUWA WATU WA
VIJIWENI WAKIENDELEZA TAALUMA YA KUVUTA HIZO BANGI AU HATA KUWA WAUZAJI
KAMA WAVUTAJI WENYEWE WANAVYOWAITA - [MAPUSHER-MEN ].
ORGANAIZESHENI YA NGUMI
ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO ] INAAMINI KABISA KWAMBA VITA VYA KUPAMBANA NA
MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA NA HATA YA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI
HAVIHITAJI MANENO MATUPU BALI VINAHITAJI USHUJAA MKUBWA NA UWAZI KATIKA
UTEKELEZAJI WAKE ,HIVYO RAIS WA TFF ANAHITAJI AWE NA MADAKTARI WENYE
UAMINFU NA AMBAO HAWATAKUWA TAYARI KUSHAWISHIWA KWA LOLOTE ILI
WAPINDISHE TARATIBU WATAKAZOELEKEZWA.
HII IKIWA NA MAANA
KWAMBA KABLA YA KUABNZA KWA MECHI ZA KILA SIKU ZA LIGI WACHEZAJI WOTE
HUSIKA NA MECHI HIYO WAPIMWE MKOJO NA DAKTARI NA BAADA YA MECHI WAPIMWE
TENA MKOJO NA DAKTARI ,HII IKIWA NA MAANA KWAMBA WAKIPMWA ASUBUHI PEKEE
INAWEZA KUTOWA MWANYA WAKATI WA MAPUMZIKO WAKAINGIA VYOONI NA KUVUTA
TENA .HIZO BANGI.
TPBO IMEKUWA MSTARI WA
MBELE SANA KTK KUPIGA VITA MATUMIZI YA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU NA YA
KULEVYA HASA BANGI NA TUMEKUWA TUKITOWA MSIMAMO WETU HADHARANI BILA WOGA
KUPITIA VYOMBO VYA HABARI ,NA HAPO MWANZO ILIKUWA NI KAZI NGUMU LAKINI
KWA KUWA NI MOJA YA KANUNI KTK NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI HATIMAYE
MABONDIA WAMEIZOWEA HALI YA KUPIMWA KABLA NA BAADA YA MAPAMBANO YAO.
NINARUDIA TENA
KUMPONGEZA RAIS WA TFF NDG TENGA KWA MTAZAMO WAKE HUU MPYA AMBAO
NIADHANI UTAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA SANA UTOMVU WA NIDHAMU WA NDANI NA
NJE YA UWANJA ,NA HATA SHERIA NA KANUNI ZA MPIRA WA MIGUU ZITAZINGATIWA
NA PIA HATA USALAMA WA WAAMUZI UTAIMARIKA HAWATAPIGWA NA WACHEZAJI. NA
HESHIMA YA MPIRA ITAIMARIKA SANA SANA.
NINATUMIA FURSA HII
KUWATAKA PIA VIONGOZI WA VILABU VYA MPIRA WA MIGUU KOTE NCHINI TANZANIA
KUMPA USHIRIKIANO MKUBWA SANA RAIS WA TFF KATIKA VITA HII YA KUPAMBANA
NA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU NA KULEVYA KATIKA MCHEZO UNAOPENDWA NA WENGI
NCHINI -MPIRA WA MIGUU.NA WAWE TAYARI KUZIPOKEA ADHABU WATAKAZOPEWA
WACHEZAJI WAO MARA WAKITHIBITIKA KUWA NA MAKOSA HAYO.
NA NJIA AMBAYO VIONGOZI
WA VILABU WANAWEZA KUFANYA KWA KUSHIRIKIANA NA TFF NI KUWAPA SEMINA
WACHEZAJI WAO MARA KWA MARA JUU YA HATARI YA MADHARA YA MADAWA YA
KULEVYA KWA WANAMICHEZO KWA KUWATUMIA WATAALAMU WALIOBOBEA KATIKA
KUELIMISHA WANANCHI HATARI ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA MADAWA HAYO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA , NA WATU WAKE WOTE
MUNGU WAEPUSHE WANAMICHEZO WOTE WA TANZANIA NA MATUMIZI YA BANGI MICHEZONI.
MUNGU UWAJAALIYE WACHEZAJI WOTE WANAOVUTA BANGI WAACHE KABLA HAWAJAFEDHEHESHWA NA VIPIMO. AMEEEEEEN
IMEANDIKWA NAMI;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH
RAIS- TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION--TPBO
No comments:
Post a Comment