Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akifuturu
pamoja na Watoto yatima wa kituo cha kulelea watoto hao cha New Life kilichopo
Kigogo jijini Dar es Slaam
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki
wakiwa na Mkurugenzi wa kituo cha Kulele Watoto Yatima cha New Life
Na Michael Machellah
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo leo
imefuturu pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Home New Life kilichopo Kigogo
jijini Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa
Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky amesema wamefanya hivyo ili kuonyesha upendo
kwa watoto hao ambao pengine kwa kipindi kama hiki wangekuwa na Wazazi wao
lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wako katika mazingira hayo na si kwa ridhaa
yao.
Alisema Chocky wao kama sehemu ya jamii
inayowazunguka watoto hao hawanabudi kufanya hivyo angalau hata Watoto hao nao
wajitambue kuwa kana jamii inawazunguka na inatambua uwepo wao.
Chocky alisema kwa mfano huo anawaomba hata Bendi
zingine waige mfano huo na si bendi tu bali hata watu binafsi kwani Watoto hao
ni wetu sote hatuna budi kuwafariji na kufurahi pamoja nao tupatapo
nafasi.
Bendi ya Exta Bongo sasa iko kwenye mazoezi makali
ikijiandaa na maonyesho ya Idd mosi na Idd pili ambapo Idd mosi wanatarajia
kufanya onyesho katika Ukumbi wao wa New White Kimara na Idd pili watakuwa
katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto Yatima wa kituo
cha New Life wakifuturu pamoja na wanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo
Mwimbaji wa Bendi
ya Extra Bongo, Rama Pentagon akigawa maadazi kwa watoto wakati wa futari hiyo
No comments:
Post a Comment