WAZIRI
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imevitaka vyama ambavyo wachezaji wake
waliiwakisha Tanzania
katika michezo ya Olimpiki kuwasilisha ripoti kuanzia jinsi walivyojiandaa,
kushiria hadi matokeo waliyopata.
Agizo
hilo limetolewa juzi usiku na Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo, katika hafla ya kuikaribisha
timu ya Olimpiki ya Tanzania
na kurejesha bendera ya taifa serikalini.
Akitoa
maagizo hayo ya Waziri, Dk. Fenella Mukangara, Mkurugenzi huyo alisema, Waziri
ameagiza viongozi wa vyama hivyo na vile vilivyokuwa katika mpango wa kusaka
viwango vya kushiriki michezo hiyo, waandae tathimini ya ushiriki wao kupitia
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuiwakilisha kwake.
“Viongozi
wa vyama, muandae tahmini ya ushiriki wenu wa Olimpiki, nini kimetokea ndani ya
miaka minne, mlifanya nini, mlikwama
wapi na nini kifanyike,” alisisitiza Thadeo kwa Niaba ya Waziri, ambaye alikuwa
akihusdhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma
na kuongeza.
Kama
mlivyosema, maandalizi yanakiwa yaanze kesho, sasa ili twende Brazil 2016
lazima tuwe tumejipanga kwa kutambua tatizo kwa kufanya tahmini na kuweka
mipango ya pamoja ikiwashirikisha washika dau mbalimbali, sio tunataka twende
Brazil wakati vikwazo bado vipo palepale.
Pia
Mkurugenzi huyo, aliwasilisha salamu za pongezi kwa wanamichezo hao, kwani
kushiriki kwao kulitokana na kufuzu vigezo na wala si kupendeleana wala
urafiki, hivyo wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao, hivyo wakaribie nyumbani.
“Mheshimiwa
Waziri, anawakaribisheni na kuwa pongeza
sana, mmekutana na mengi sana ya ‘kuwa- discourage’ lakini mmepambana, mengi
yametokea, hamkwenda huko kwa utashi wa mtu, mmepita katika vigezo, ni jambo la
kujivunia mevipita vigezo na si urafiki, tuchukulie kama chachu tukifanua
vizuri tutapongezwa tu,” alisema.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Rais wa TOC, Ghulam Rashid, matokeo hayo yametokana
na aina ya maandalizi yaliyofanywa na vyama kwa kushirikiana na Kamati ya
Olimpiki (TOC), huku akiwataka Watanzania kutatambua kwamba ili kupata
mafanikio katika mashindano ya kimataifa, inahitajika maandalizi na vifaa vya
uhakika, vitu ambavyo viko juu ya uwezo wao, hivyo kila Mtanzania anatakiwa
kusaidia kwa hali na mali.
“Tunaomba
Watanzania waelewe, ili mchezaji afanye vizuri inahitajika maandalizi ya
uhakika nay a muda mrefu na vyama vyetu ni malofa, haviwezi pekee yao, hivyo tuna wajibu wa kuvisaidia
ili viweze kuwaandaa vema na hatimaye kuja kufanya vema,” alisema Ghulam.
Katika
Olimpiki London 2012, Tanzania iliwakishwa na wanamichezo sita, ambao ni
wanariadha, Samson Ramadhani ambaye alikuwa nahodha, Faustine Mussa, Zakia
Mohamed na Mxsenduki Mohamed ambaye hata hivyo hakukimbia baada ya kushikwa na
nimonia, bondia Selemani Kidunda, waogeleaji Magdalena Moshi na Amaar Ghadhiar.
No comments:
Post a Comment