Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Malawi Mh
Joyce Banda nchini Msumbiji, ambapo wameelezea nia ya nchi zao kufikia
suluhu kwa njia za Kidiplomasia kupititia Kamati Maalumu iliyoundwa
kushughulikia mgogoro huo (Picha na Freddy Maro).
MAPUTO, Msumbiji
RIS Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na
mwenzake wa Malawi, Joyce Banda, wamekutana nchini Msumbiji na kufanya
mazungumzo mafupi yenye nia ya kumaliza mgogoro wa mpaka unaohusisha
nchi zao.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na
Joyce Banda walikubaliana kumaliza mgogoro huo Kidiplomasia, kupititia
Kamati Maalumu iliyoundwa kushughulikia sakata hilo linalohusu mpaka
sehemu ya Ziwa Nyasa.
Kupitia mazungumzo hayo, Rais Kikwete
alisema: "Mimi ndiye Amir wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania,
sijapanga wala kutoa agizo la vita...
"Wanasiasa na waandishi wa habari wa
mataifa yote mawili, wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki
na chokochoko miongoni mwa raia, hasa wa maeneo ya mpakani.
Rais Kikwete akaenda mbali zaidi kwa
kutaka: "Watanzania na Wamalawi, muyapuuze maneno hayo, badala yake
acheni Diplomasia ifanye kazi yake,"
No comments:
Post a Comment