Mh.Lowassa akiangalia madawati yaliyokabidhiwa kwa shule hiyo na Benki ya KCB hivi karibuni.
Waziri
Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akikabidhiwa kibuyu na mama wa kimasai
kata ya Mkundi wilaya ya Morogoro.Mh.Lowassa ni kiongozi wa jamii ya
wamasai nchini.
Waziri
Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwasalimia wanafunzi wa shule ya
msingi ujirani katika eneo la wafungaji wa jamii ya wamasai kata ya
mkundi wilaya ya Morogoro alikokwenda kukagua na kukabidhi harambe za
wafugaji hao kwa ajili ya ujenzi wa shule yao hiyo.
**** **** ****
Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa ameuomba uongozi wa mkoa wa Morogoro kulishughulikia tatizo la uchomaji moto misitu.
Akizungumza
mapema leo kwenye kijiji cha Kiegea mjini Morogoro,Mh.Lowassa ametoa
wito huo alipokuwa akikabidhi michango ya harambee ya wafugaji wa jamii
ya Wamasai,kusaidia ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo.Mh Lowassa
alialikwa kufanya kazi hiyo akiwa ni kiongozi wa jamii ya wamasai
nchini.
Mh.Lowassa
pia aligusia suala la baadhi ya wanchi kuwa na tabia ya kuchoma moto
misitu hovyo hasa mkoa wa Morogoro,hali inayopelekea uharibifu mkubwa wa
Mazingira,Lowassa amebainisha kuwa kila anapopita mkoani morogoro
amekuwa akishuhudia misitu ikichomwa moto,hali iliyokuwa ikimhudhunisha
sana.
''Nimekuwa
nikishuhudia maeneo kadhaa ya misitu yakichomwa moto,kwa hivyo ndugu
zanguni naomba tuachane na tabia hii pamoja na kuwa kilimo ni muhimu
katika maisha yetu ya kila siku,lakini kwa njia hii tutaufanya mkoa huu
wa Morogoro ugeuke jangwa'' alionya Lowassa na kuongeza kuwa iwapo
mwanamuziki maarufu wa mkoa huo, Marehemu Mbaraka Mwinshehe angefufuka
angesikitika sana.
''Mara
nyingi nikikutana na hali hii,huwa naukumbuka wimbo wa Mbaraka
Mwinshehe unaosema kuwa Morogoro maji yatiririka milimani, kama
akifufuka atalia'' alisema Lowassa na kuuomba uongozi wa mkoa
kushirikiana kwa pamoja kutafuta suluhisho la tatizo hilo ambalo
limekuwa likikithiri siku hadi siku.''Mh DC wa Morogoro nawaombeni
mtafute suluhisho la tatizo hili, tusipoangalia mkoa huu utakuwa
jangwa''alisema.
Aidha
Mh.Lowassa amesema kuwa suala la elimu ni muhimu zaidi kabla ya kilimo
kwanza,akaongeza kuwa Elimu kabla baadaye kilimo kwanza.Mh Lowassa pia
ametoa changamoto kwa wananchi wa kata mpya ya mkundi ya jamii hiyo ya
wafugaji kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.
''Ni
aibu kata hii kutokuwa na shule ya sekondari wakati kila kata nchini
ina shule ya sekondari ,ambako hivi sasa angalau kuna usawa kwa watoto
kugusa elimu ya sekondari'' alisema na kuongeza kuwa atakuwa tayari kuja
kwenye kata hiyo Januari mwakani kuongoza harambee ya kuchangisha
fedha za ujenzi wa sekondari.Mh.Lowassa ndiye aliyeongoza operesheni ya
ujenzi wa shule za kata kote nchini wakati alipokuwa waziri mkuu.
''Niko
tayari kuja January kuongoza harambe ya kuchangisha fedha, ni aibu
kwakweli sijafurahishwa na hali yenu hapa mnatakiwa nyinyi wenyewe
msimame kidete kujiletea maendeleo, njooni Monduli mjifunze jinsi
wafugaji wenzenu walivyoweza kutumia mifugo yao kujenga shule na nyumba
za waalimu'' alisema Lowassa.
Mh.Lowassa
amemtaka kila mfugaji kutoa ng'ombe au mbuzi mmoja kwa ajili ya
kuchangia elimu kwenye kata yao na kumuomba mkuu wa wilaya kutumia
sheria zilizopo kumkamata na kumtia ndani yeyote atakayekaidi wito huo.
Mh
Lowassa alichangia mabati 500 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa
madarasa ya shule hiyo ya msingi ya Ujirani yenye wanafunzi 414 ,lakini
yenye upungufu mkubwa wa Waalimu, wawili tu mmoja wa kuajiriwa na
mwingine wa kujitolea.
Katika
harambee ya wananchi wa eneo hilo walichanga ng'ombe watano kwa ajili
ya kuendeleza shule hiyo, idadi ambayo mh Lowassa aliipinga,akidai kuwa
ni Wanachi hao wana idadi kubwa ya mifugo hivyo walipaswa kujitolea
zaidi.
No comments:
Post a Comment