Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 17, 2012

MASHUJAA MUSICA NA RATIBA YAO YA SIKUKUU YA IDD EL FITRKiongozi wa Mashujaa Musica, Charlz Baba

BAADA ya kukamilisha ziara ya kutambulisha wanamuziki wake wapya wa Mashujaa Band, sasa ni zamu ya kuwapa burudani wapenzi wa bendi hiyo kwa siku ya Idd Mosi na Idd Pili.
Meneja wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd mosi watakuwa Msasani kwenye ukumbi wa Emirates.
Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd pili watakuwa Mjini Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Bendi hiyo ambayo hivi sasa ipo hivi chini ya Rais wake Chalz Baba, itatoa burudani hiyo kwa ajili ya kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa nyimbo zao na Bendi yao kwa ujumla.
Alisema, pia kwa wale wanaoisikia Bendi ya Mashujaa kwenye vyombo vya Habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo laivu katika Sherehe za Eid El Fitri.
“Kama tulivyowapagawisha wakazi wa Songea na Mbeya wiki iliyopita, sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mtwara,” alisema Sospeter.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...