Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Yanga wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana wakitokea katika
ziara ya michezo ya kirafiki nchini Rwanda
NaMwandishi Wetu
MASHABIKI wa soka nchini wameendelea kutoamini macho yao,
baada ya Mabingwa wa Soka Afrika Mashariki na Kati Yanga leo kutua
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam
ikitokea Kigali, Rwanda, bila ya beki wake mpya aliyecheza mechi za kirafiki nchini humo Mbuyu Twite.
Twite aliyesajiliwa na Yanga akiwa Rwanda
na kisha kubaki huko hadi alipoungana na timu nchini humo na kucheza
mechi hizo za kirafiki, alitarajiwa kutua jijini na Wanajangwani hao,
ambapo mashabiki wa Yanga na wa Simba walisubiri ujio wake.
Kusubiriwa kwa
hamu kwa Twite kunatokana na mkanganyiko aliozua katika usajili wake,
ambapo awali alisajiliwa na kutambulishwa na Simba akitokea APR ya Rwanda alikokuwa akicheza kwa mkopo, kabla ya Yanga kutibua dili hilo na kumsainisha kupitia klabu yake ya zamani ya Lupopo ya DRC.
Licha ya kutowasilisha jina lake kwa
TFF, Simba imeendelea kulia na Twite iliyemtangaza kuwa tapeli na
kumfungulia jalada (RB) la wizi wa kuaminika wa dola za Kimarekani
30,000 za usajili, huku ikimtaka kurejesha fedha hizo mwenyewe kama alivyopewa.
Akizungumza na
waandishi wa habari uwanjani hapo wakati msafara wa watu zaidi ya 40
Yanga, wakiwamo wachezaji 28 ulipopokelewa, Katibu Mkuu wa Yanga
Mwesigwa Celestine, alisema kuwa, Twite atawasili nchini wakati wowote
na kuwa amebaki Kigali akikamilisha baadhi ya mambo.
“Hakuna cha
kumtish Twite kiasi cha kutoungana nasi kuja Dar, kuna taratibu muhimu
anashugulikia. Atatua nchi wakati wowote na tutakuwa naye katika pambano
letu na Coastal Union hapo Jumamosi,” alisema Mwesigwa akikana habari zilizozagaa uwanjani hapo kuwa alihofia kutiwa mikononi na Simba.
Katika mechi
ya kwanza, Yanga iliyokuwa pia icheze na APR katika mechi hizo,
iliichapa Rayon Sport mabao 2-1, shukrani kwa mabao ya washambuliaji
Hamisi Kiiza na Simon Msuva, kabla ya juzi mabeki Stephano Mwasyika na
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuipa ushindi dhidi ya Polisi.
Kocha Tom
Saintfiet kwa upande wake alifurahishwa na ziara hiyo, akisema kuwa
anaamini vipimo bora kuitoka kwa Rayon na Polisi, vimesaidia
kuwaimarisha vijana wake, kuelekea Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa
kuanza mwezi ujao.
“Licha ya
kukosa fursa ya kuumana na APR, lakini najivunia changamoto ilizopata
timu yangu kutoka kwa Rayon na Polisi. Ni timu bora na imara zilizotupa
makali stahili na sasa tuko tayari kwa ligi,” alisema Saintfiet.
Msafara huo
uliongozwa na Mwenyekiti, Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ambao ni Mama Fatma Karume, Francis
Mponjolwe Kifukwe na Seif Magari, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji, Abdallah Bin-Kleb na Salum Rupia.
Mbelgiji
Saintfiet, na Msaidizi wake Fred Felix Minziro, waliongoza benchi la
ufundi lililojumuisha pia kocha wa makipa, Mfaume Athumani, Meneja
Hafidh Saleh, Daktari, Sufiani Juma na mtunza vifaa Mahmoud Omary
No comments:
Post a Comment