Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 31, 2012

SERENA APAA, VENUS WILLIAMS AKIAGA US OPEN 2012



NEW YORK, Marekani

Wakati Serena akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber

NYOTA anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa tenisi duniani, Serena Williams hakupata shida kufuzu raundi ya tatu ya micuano ya Wazi ya Marekani ‘US Open’ baada ya kupata ushindi wa moja kwa moja dhidi ya Mhispania Maria Jose Martinez Sanchez.

Bingwa huyo wa michuano ya Wimbledon na Olimpiki, alitumia muda wa saa moja na dakika 22 (1:22) kuibuka kidedea kwa seti mbili kwa bila za 6-2 6-4 dhidi ya nyota asiyekuwa na kiwango Sanchez.

Wakati nyota huyo akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber.

Nyota namba mbili kwa ubora duniani, Agnieszka Radwanska alilazimika kufanya kazi ya ziada kutoka nyuma na hatimaye kumshinda Mhispania Carla Suarez Navarro kwa 4-6 6-3 6-0.

Kwa upande wake mkali wa mchezo huo raia wa Serbia, Ana Ivanovic aliibuka kidedea na kutinga raundi ya tatu ya michuano hiyo kwa ushindi wa 6-2 6-2 dhidi ya Msweden Sofia Arvidsson.

Katika raundi ya tatu, Ivanovic anatarajia kupata upinmzani mkali kutoka kwa yoso wa miaka 19 Sloane Stephens, yoso aliyeingia katika 50 bora ya wacheza tenisi wanamama, aliyetinga hatua hiyo kwa kumchapa Tatjana Malek wa Ujerumani kwa 5-7 6-4 6-4.

Licha ya kutupwa nje ya mashindano, bingwa mara tano wa Wimbledon Venus alisema; "Nilijihisi Marekani kwa mara ya kwanza " kutokana na aina ya sapoti aliyooneshwa na kutoka kwa mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa Arthur Ashe.

"Hii ni mara ya kwanmza ambayo nimecheza hapa na kuona kundi kubwa la mashabiki likiwa nyuma yangu kama hivi. Nilisubiri uungwaji huu kwa muda mrefu, hatimaye nimeupata ingawa matokeo hayakuwa mazuri," alisema Venus.

"Ilikuwa ya kushangaza sana. Nilijisikia kama niliyeshinda dhahabu. Kiukweli ilimaanisha kitu. Kwa sasa naangalia mbele kuona namna navyoweza kutumia ipasavyo sapoti mara mbili yah ii niktakayopata katika michuano ya mwaka ujao nikiwa bora zaidi."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...