Miss East Africa Ethiopia-Lula Teklehaimanot (19)
Miss East Africa Seychelles-Annabelle Marvel Pointe (19)
Miss East Africa Uganda-Ayisha Nagudi (23)
MISS EAST
AFRICA 2012
PRESS RELEASE 26/08/2012
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE
kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia
million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.
Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi
ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa
imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata wawakilishi
wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa
na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za
ukanda wa afrika mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa
kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan,
Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar,
Reunion, Comoros,
na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano
na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania
kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.
Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo
zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni Eritrea,
Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia
zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni
tarehe 28 mwezi September.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment