Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka
(kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na
Makazi, lililoanza leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro,
wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa
Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya
kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kukamilisha
zoezi la kujibu maswali husika katika zoezi hilo, leo asubuhi nyumbani
kwake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa
Kituo cha Oysterbay, Daria Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya
Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe.
**************************************
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa
ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Dkt.
Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa
akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye
alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria
Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu, Stanley Mahembe na
Radegunda Maro.
Katika
zoezi hilo, Dkt, Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali
37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo, yaliyokuwa yakiulizwa na
Karani Happyness Masaka.
Akizungumza
baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote
kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha
zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
No comments:
Post a Comment