Mkufunzi
wa masuala ya aundaaji wa Filamu kutoka taasisis ya Sanaa na uandishi
wa Habari (IAMCO) Ngalimecha Ngahyoma, akizungumza jambo katika Jukwaa
la Sanaa, kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa
na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na kushoto ni Katibu Mtendaji wa
BASATA Ghonche Materego
Na Mwandishi Wetu
Wasanii
wa nchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze
kufanya kazi zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na
nje ya nchini.
Akizungumza
katika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu
hapa nchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi
katika uandaaji wa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii
kutokuelewa misingi ya uandaaji wa filamu.
“Kuna
maeneo ya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa
utimilifu, na hakuna njia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana
lazima mtu ufundishwe. Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini
matokeo ya kufanya mambo kwa vipaji ndiyo haya ambayo yanatupa filamu
zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,” alisema.
Alisema
ni muhimu kwa wasanii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake
kuanza kuandaa kazi kitaalamu ili kufanya kazi zilizobora na kwamba ni
vyema kutumia wataalam katika maeneo yote yanayohitaji utalaam badala ya
mtu mmoja kufanya kazi zote.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Ghonche Materego, amesema suala la taaluma alikwepeki katika kutengeneza
kazi zenye ubora na kuwasisitiza wasanii kujiunga na vyuo kupata
utaalam katika fani zao.
No comments:
Post a Comment