Kundi
la SKYLIGHT Band likishambulia Jukwaa kabla ya uzinduzi wa Kinywaji
Kipya kinachozalishwa na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) cha
MALTIZA kinachotengenezwa na Kimea halisi kisicho na kilevi uliofanyika
katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar leo.
Malkia
wa SKYLIGHT Band inayokuja kwa kasi jijini Aneth Kushaba (mbele kulia)
sambamba na Mariam Lucas wakikonga nyoyo za Wakazi wa Dar waliohudhuria
uzinduzi huo.
Meneja
wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata
Adam (katikati) akikaribisha wageni kuhudhuria uzinduzi wa kinywaji
hicho uliofanyika leo jijini Dar.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakiorodhesha majina yao kwa warembo maalum
waliondaliwa kupokea wageni na kushiriki bahati nasibu ya papo kwa hapo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha MALTIZA.
Meneja
wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata
Adam akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa
kinywaji hicho kipya kinachopatikana katika ladha mbili za APPLE na PINE
(Pineapple) ambacho amefafanua kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kwa
Afrika kuzindua kinywaji cha aina hiyo kisicho na kilevi chenye ubora na
kinachotengenezwa na kimea halisi kinachozalishwa hapa nchini.
Bi.
Consolata Adam amesema kinywaji hicho kinapatikana katika ujazo wa
330Mls na kimeshasambazwa nchini kote na bei yake ni shilingi 1500,
aliongeza kuwa kinywaji hicho ni halisi kisichotiwa rangi na kuwataka
Watanzania kujiburudisha na MALTIZA.
Bi. Consolata Adam akionyesha kopo za Ujazo wa 330Mls za kinywaji cha MALTIZA aina ya APPLE na PINE.
No comments:
Post a Comment