SHINDANO la ‘Bibi Bomba’ ambalo lilikuwa likiratibiwa na kituo cha
Clouds TV, usiku wa kuamkia leo limefikia tamati na Veronica Mpangala
akiibuka mshindi wa kitita cha 5,000, 000/= (milioni tano) huku nafasi
ya pili ikitwaliwa na Anna Saidi ambaye alijipatia kiasi cha shilingi
milioni tatu, na ukurasa wa washindi ukifungwa na Nasra Mohamed ambaye
alijitwalia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.
Washiriki wengine watano ambao walikuwa wamesalia kwenye shindano hilo
walipatiwa zawadi kila mmoja na watu mbalimbali waliokuwa wamealikwa kwa
ajili ya kufanikisha zoezi hilo.


No comments:
Post a Comment