LONDON, England
MBIO
ndefu za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya England zinaanza rasmi kesho,
ambapo klabu 14 kati ya 20 za ligi hiyo zitajitupa kwenye viwanja
mbalimbali, kuwania pointi tatu muhimu katika siku hii ya ufunguzi.
Pazia
la ligi hiyo lililofunguliwa wiki jana kwa pambano la Ngao ya Jamii
baina ya mabingwa watetezi Manchester City na mabingwa wa Kombe la FA,
Chelsea, litashuhudia muendelezo wake hapo kesho-kutwa Jumapili na
Jumatatu usiku.
Klabu
iliyoipa Man City ubingwa katika dakika za mwisho za siku ya kuhitimisha
ligi msimu uliopita QPR, itakuwa nyumbani kuumana na Swansea, huku
Reading iliyorejea Ligi Kuu ikishuka kwenye uwanja wa nyumbani kuwaalika
Stoke City.
Washika
Bunduki walio kwenye sikitiko la kumpoteza mkali wake Robin Van Persie,
wanaanzia nyumbani Emirates kesho, kwa kuwaalika Sunderland, huku
Wekundu wa Anfield Liverpool wakisafiri kuwafuata West Brom.
Wagonga
Nyundo wa London, West Ham United, wataumana na Aston Villa, huku Fulham
ikitarajiwa kushuka kwenye dimba la Craven Cottage kupimana na ubavu na
Norwich City, mechi zote hizo zinatarajiwa kuchezwa saa 9:00 alasiri
(sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki).
Pambano
linalotazamwa na wengi hapo kesho litapigwa 11:30 (sawa na saa 1:30
Afrika Mashariki), ambapo Newcastle United watakapowakaribisha Tottenham
– inayonolewa na kocha Andre Villas-Boas.
Jumapili
watetezi Man City wanatarajia kutupa karata yao kwanza hapo kwa kuumana
na Southampton kwenye Uwanja wa Etihad, huku Wigan ikiwa nyumbani
kuwapima wabingwa wa FA waliolala katika Ngao ya Jamii, Chelsea.
Mechi za
ufunguzi wa ligi hiyo zitahitimishwa Jumatatu usiku, wakati Manchester
United watakapoumana na Everton pambano linalotarajiwa kuwa la kwanza
kwa Mholanzi Van Persie, aliyekamilisha uhamisho wa kuchezea United
akitokea Gunners.
No comments:
Post a Comment