Kombaini
ya Copa Coca-Cola Tanzania (Dream Team) yenye wachezaji 16 inatarajia
kuondoka kesho (Agosti 28 mwaka huu) asubuhi kwenda Afrika Kusini kwenye
kambi itakayokuwa chini ya makocha wa Chelsea.
Makocha
watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo watakaoongoza kambi
maalumu ya kimataifa ya Copa Coca-Cola yenye wachezaji 140 kutoka nchini
15 itakayofanyika jijini Pretoria kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8
mwaka huu.
Robert
Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason
Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo
wanaounda jopo hilo la makocha litakalowanoa vijana hao wenye umri chini
ya miaka 17.
Wachezaji
wanaounda Dream Team iliyotokana na michuano ya Copa Coca-Cola
iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 24 hadi Julai 15 mwaka
huu ni Abrahman Said Mohamed (Zanzibar), Ayubu Alfan (Dodoma), Baker
Hamad (Tanga), Edward Joseph (Ruvuma), Hassan Kabunda (Temeke) na Joseph
Chidyalo (Dodoma).
Wengine ni Mtalemwa Katunzi (Morogoro), Mwarami Maundu (Lindi), Nankoveka
Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Rajab Rashid (Mwanza), Said
Ramadhan (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke),
Tanganyika Suleiman (Kigoma) na Tumaini Baraka (Kilimanjaro).
Nchi
nyingine zitakazokuwa na washiriki katika kambi hiyo ni wenyeji Afrika
Kusini, Burundi, Cameroon, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC), Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Swaziland,
Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Hii
ni mara ya sita mfululizo kwa kampuni ya Coca-Cola kupeleka Dream Team
kwenye kambi za kimataifa. Mwaka 2007 na 2008, timu hiyo ilikwenda
Brazil wakati mwaka 2009, 2010 na 2011 ilikuwa Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment