Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 4, 2013

ECOBANK KUPUNGUZA GARAMA ZA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata taarifa kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Yuquing wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.  
Ofisa mauzo wa Ecobank Jakline Nyangoe (kushoto) akifafanulia jambo wageni waliofika katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Februari 3 2013.
 Wakazi wa Dar es Salaam na wageni mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
W
akazi wa Dar es Salaam na wageni mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
*********************************
Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki  biashara kati ya Tanzania naChina kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.

Wakishiriki katika sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Ecobank ilionyesha nia yake ya kusaidia jamii ya waendesha biashara kati ya Tanzania na China zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara wa Tanzania na wawekezaji wa Kichinakushiriki katika uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi hizi.

 "Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi sana. 

katika mwongo uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa china ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara hii "anasema Bw EnochOsei-Safo, Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.

Ecobank inazindua huduma ya kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB) moja kwa moja, ambapo hapo awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola za kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara walipoteza kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha wanabiashara kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa Tanzania.
" Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara ya China juu ya Afrika, ambayo inafikia zaidi ya dolabilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji na 5% ya mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa kifedha kukuza sekta hii ni muhimu, na ndiyo maana Ecobank Groupimeonyesha nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha Afrika kuwa na ushindani na nchi zingine duniani.” Enoch aliongeza.

Ecobank Tanzania katika miezi michache ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za uendeshaji biashara kati ya Tanzania na China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi ya forodhani kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote ya Ecobank. 
Kwa maelezo zaidi, tembelea: www.ecobank.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...