Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumzia mwamko wa watanzania
katika kujitolea kufanya usafi ambapo amesema, bado ni mdogo ndio maana
tulisema wakati ule tunaanza mwezi wa saba tutumie karibu miezi mitatu
tutoe elimu, lakini tumeongeza miezi mitatu mpaka Desemba na tukaongeza
miezi mingine mitatu mpaka Machi, tutoe elimu ili ifike wakati watu wote
waone ni majukumu yao kuhakikisha mji uko safi.
Amesema
kuwa wamefanya kampeni hii Usafi kuanzia Kata ya Kivukoni na leo Kata
ya Kisutu na wiki ijayo wanatarajia kuwa Kata ya Mchafukoge.
Ameongeza
kuwa sasa tumeona iko haja ya kuanza kutekeleza sheria, hivyo tunafanya
kampeni hizi tukiwa na askari wetu wa jiji na pale tutakapoona mtu au
sehemu inatuchafulia mazingira kwa makusudi basi askari watatumika. Mstahiki
Meya amesema anaamini kama kila mtu anaweza kuoga mwili wake, kusafisha
nyumba yake basi anaweza kuyaweka safi mazingira yanayo mzunguka.
Meneja
Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena
akizungumzia kampeni hizo za usafi amesema zilianza tangu tarehe 19
Januari katika Kata ya Kivukoni ambapo watu wamejitokeza kwa wingi sana
na kufanikiwa kutoa taka nyingi sana katika maeneo ya ufukweni.
Amesema
ni kitendo cha kushukuru kuwa watu sasa hivi wanaelewa na kuanza
kushiriki katika suala zima la mazingira na pia kuna viongozi wengi
wameacha shughuli zao wakaja kushiriki katika kampeni hii ya usafi hivyo
zoezi hili likitoka hapa litahamia Kata ya Mchafukoge.
Baada
ya kuhitimisha zoezi hilo katika kata hizo tunataka liwe zoezi
endelevu, hatutaki liwe la nguvu za soda kama wengine wengi wameanzisha
mikakati kama hii baadae wameishia kwenye makapu, sisi tutaanzisha
vipindi katika Television lakini pia katika tarehe za katikati hapa
tumeanzisha program ya elimu mashuleni.
Amesema
wameanza na shule ya Bunge ambapo amesema katika hatua inayofuata
watafanya program na wanafunzi kwa lengo la kusambaza elimu miongoni mwa
wanafunzi.
Afisa
Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Samuel Bubegwa (kushoto) akiwa na
viongozi wa kata ya Kisutu kabla ya kuanza zoezi la kusafisha mazingira
katika kata hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa kwanza kushoto)
akiongoza umati wa wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro ltd, wadau
wa mazingira, maafisa wa manispaa ya Ilala na wakazi wa kata ya Kisutu
wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira lilioendeshwa na kampuni
ya Green Waste Pro ltd katika maeneo ya kata hiyo ikiwemo mitaro,
barabara na maeneo ya wazi na kwingineko.
Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie (wa kwanza kushoto) akishiriki zoezi hilo.
Umoja ni Nguvu Utengano ni Dhaifu.........zoezi la kufagia barabara zinazoizunguka kata ya Kisutu likiendelea.
Moja ya magari ya kisasa ya kampuni ya Green Waste Pro ltd likifagia barabara kwa kutumia Teknolojia inayoenda na wakati.
Barabara ya mzunguko wa DTV ikifagiliwa.
Vijana wakichapa kazi.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akimkemea mmoja wa wafanyabiashara ya Chai pembezoni
mwa barabara karibu na maeneo ya DTV anayeosha vyombo na kumwaga maji
yenye uchafu barabarani.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimuonya kuacha tabia hiyo na kumtaka
kufuata utaratibu wa kutunza mazingira kama unavyoelekezwa na manispaa
ya Ilala na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiunga
mkono zoezi la usafi katika maeneo ya Kata ya Kisutu Uhindini jijini Dar
leo.
Mstahiki
Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kushoto), Mwanasheria wa
Manispaa ya Ilala Paul Wanga na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala
Samuel Bubegwa wakivuta pumzi baada ya kupigika na kazi ya kusafisha
maeneo ya Kisutu.
Mstahiki Meya Jerry Silaa na viongozi wa manispaa ya Ilala wakifagia korido za majengo ya maeneo mbalimbali ya Kisutu.
No comments:
Post a Comment