Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 5, 2013

SAMSUNG YALETA UHAKIKA NA MFUMO WA “E-WARRANTY”.


 Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za Samsung, Lawrence Andrew wakichezesha droo ya mwezi kwa wateja wa bidhaa za Kampuni hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
 Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za Samsung, Lawrence Andrew wakimpigia mteja aliyeshinda kwenye droo ya mwezi kwa wateja wa bidhaa za Kampuni hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara(wa tatu kushoto) akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam namana  ya droo inavyochezesha na washindi wanavyopatikana wakati wa kuchezesha droo ya mwezi iliyochezeshwa Mwenge Dar es Salaam jana.

Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Samsung Tanzania imechezesha droo ya mfumo wake wa “E-Warranty”, washindi walitangazwa katika hafla iliyoandaliwa katika Stendi Kuu ya Mwenge, jijini Dar es Salaam. Mfumo huu wa “E-Warranty ni mbinu inayotumiwa na Kampuni ya Samsung kama jinsi ya kukumbana na bidhaa feki zinazopatikana kwenye soko la Tanzania.
Mfumo huo wa e-warranty unawasaidia wateja kujua kama simu ya Samsung ni halali au ni feki. Wateja wanapaswa kusajali simu zao pale wanapozinunua na hivyo kupata dhamana ya miezi 24.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema “Mfumo wa E-Warranty imeonyesha kwamba ni mbinu bora zaidi dhidi ya kukumbana na bidhaa feki kwani wateja wengi wanasajili simu zao. Tunawahimiza wateja wetu  waendele kutuunga mkono kwa kununu bidhaa bora na kuzisajili na hivyo kupata nafasi ya kujishindia bidhaa kabambe za Samsung katika droo zetu”.
Washindi wanaweza kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10: Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32, laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na simu 2 aina ya Galaxy Grand.
Bwana Kumar aliendelea kusema “ Licha na kujua kama simu mteja anayotaka kununua ni bora au feki, mfumo wa e-warranty unawasiadia wateja kujua kama simu hiyo inadhama ya miezi 24, kama simu hiyo inatafutwa au imeibiwa na kama simu hiyo ni mpya au imeshatumika”.
Kujua kama simu ni halali, mteja anatakiwa kufuta maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’ ikifuatiwa na alama ya nyota (*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa na alama ya reli (#) na kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa moja kwa moja kuelezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung.
“Mfumo huu wa e-warranty ulianzishwa haswa kukabiliana na changamoto moto inayoikumba soko la simu za mkononi huku Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu nyingi ni za bandia, za wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana”, alisema Bwana, Kumar.
Bwana Kumar alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4 (iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa ADH. ADH (Accidental Damage from Handling), ni huduma inayoilinda simu hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na matumizi ya kawaida’.
Ilikujiunga na huduma ya ADH, wateja wanatakiwa kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili untakiwa kufanywa ndani ya siku 30 tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure pale ambapo itaharibika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...