Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 2, 2013

Watanzania wanaonunua Bidhaa halisi waendelea kupongezwa katika Promosheni ya Pambika na Samsung


Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akiongea na mmoja ya washindi wa promosheni ya Pambika na Samsung wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung. Washindi 15 walipataikana katika droo hiyo ambapo baadhi ya washindi walikuwa ni Issa Richard Moshi (23), wa Kilimanjaro aliyejishindia deki ya DVD, Agnes John Mkalango (30) wa Mwanza, Adagoti Komba (57) wa Dodoma, Faustine Kirusya (45) mkazi wa Mbeya ambae ni askari polisi pamoja na Praygod Amos (39) wa Arusha wote wameshinda Muziki wa Nyumbani. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein.
 Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akijadiliana jambo na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein Wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung mapema hii leo. Zawadi kubwa kabisa ya wiki hii ilikuwa ni Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 ambapo mshindi wake ni Bi.  Bernadeta Peter mkazi wa Dar es Salaam huku Bi. Anthonia Julius Masele (45) ambae amejinyakulia luninga ya LED ya Samsung ya inchi 32 wa Dodoma. Hamad Abdallah Hemedi wa Dar es Salaam ambae amejinyakulia kompyuta mpakato.
Kutoka kulia ni Bw. Humudi Abdulhussein toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, katikati ni Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na Chacha Magege wakifuatilia droo kwa makini wakati wa kuchezesha droo ya Pambika na Samsung.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...