RAIS wa Shirikisho la Soka
nchini (TFF) Jamal Malinzi amesema watakaa na wadhamini wa mashindano ya Uhai
ili yachezwe kwa mfumo wa ligi, sambamba na ligi Kuu ya Tanzania Bara
Malinzi aliyasema hayo juzi
wakati akifunga fainali za mashindano ya kombe la Uhai zilizofanyika katika
Uwanja wa Chamazi ulionje ya jijini la Dar es Salaam.
“Tunawapongeza Uhai kwa
kufadhili mashindano haya ambayo yanalengo la kuibua vipaji ila shirikisho
litakwenda kuzungumza nao ili mashindano haya yachezwe kwa mfumo wa ligi
sambamba na ligi kuu ya Tanzania ili kutoa wigo mpana kwa vijana kuonyesha
uwezo wao”, alisema Malinzi.
Pia alisema mfumo wa sasa wa
makundi unazikosesha fursa timu zingine kuendelea mbele kwani inawezekana
kabisa kama mchezo wa kwanza timu inafungwa mchezo wa pili inafanya vizuri.
Katika fainali hizo timu ya
Coastal Union ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Yanga mabao 2-0 na kuzawadiwa
kikombe na fedha taslimu 2, 500, 0000 huku Yanga wakiambulia 1,500,000.
Pia Azam Fc ilichukua nafasi
tatu na kuzawadiwa 1,000,000 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar penati 4 kwa 3
baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika muda wa dakika 120.
Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alipata zawadi ya kocha bora huku Ally Kabunda wa Ashanti United akipata zawadi ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao 9 na Ruvu Shooting ikipewa zawadi ya timu bora.
No comments:
Post a Comment