Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, March 2, 2014

BAADA YA YANGA KUSHANGILIA BAO MASHABIKI WANG'OA VITI TAIFA


Katika hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wameanza tena kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupiana  uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.

Lakini kwa hali ilivyo hivi sasa Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa, kwani kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na Othman Michuzi wa MICHUZI MEDIA GROUP.


Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.

Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.

Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.

Askari Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa Mashabiki wa Simba.


Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...