BONDIA Fransic Miyeyusho ' Chichi Mawe' baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwizi hivi karibuni na Bondia
Sukkasem
Kietyongyuth
kutoka Thailand na kupelekwa hospital na kupatiwa huduma ya kwanza
kwa kufanyiwa uchunguzi wa kina sasa
itamlazimu akae pembeni bila kufanya mazoezi ya aina yoyote pamoja na
kazi ngumu katika kipindi cha mwezi mzima ili aweze kurudi katika hali
yake ya kawaida baada ya kichwa chake kupigwa ngumi nyingi kali kwa
mfululizo
akizungumzia
mpambano wake huo na mthailand huyo chichi mawe amesema mpambano huu
umekuwa ukisogezwa mbele kila wakati na nikibadilishiwa mpinzani kila
siku mara ya kwanza mpambano huu ulikuwa ufanyike mwanzoni kabisa mwa
mwaka huu ikashindikana nikambiwa nakuja kupigana na Ronald Pontillas raia wa Ufilipino nayo ikaota mbawa nikambiwa tena napigana na bondia mwingine pia ikawa hivyo hivyo
ndio nika letewa huyu mthailand kwa
sasa ata hivyo mpambano ulikuwa ufanyike april 12 ikasogezwa mbele mpaka
april 19 ndipo nilipo panda ulingoni hivyo mpambano ulikuwa na mizegwe
sana mana kila siku mkataba ulikuwa ukisogezwa mbele kwa kutumia mkataba
hule hule
aliongeza kwa kusema anaomba mashabiki
wake wamsamehe kwa kilichotokea kwa kupoteza mpambano huo kwani hata
promota mwenyewe alikuwa mbabaishaji na nilikuwa nabadilishiwa ata
mapromota mara Jay Msangi mara Mussa Kova hivyo nilikuwa sijui promota
alisi ni nani wakati mwanzo nilikuwa namjua msangi
naomba watanzania wenzangu waniombee duwa kwani mchezo kuna kupigwa na kushinda nita hakikisha siwakatishi tamaa
mashabiki wangu pindi nitakapokuwa sawa kwa kurudia ali yangu na kuanza mazoezi
hata hivyo nasikitika
kusema mpambano wangu uliokuwa ufanyike mei 10 kuzipiga na Mohamed
Matumla nitamuomba promota Ally Mwazoa apeleke mbele kwani sito kubali
kupoteza mpambano huo kirahisi najua mwazoa ametumia galama nyingi sana
kutangaza mpambano wangu na Matumla sina budi kumuomba msamaha kwa
yaliyotokea kwa kuwa yeye ni mwanamichezo na anajua madhala ya mchezo wa
ngumi atanielewa kwa kulisogeza pambano hilo mbele
No comments:
Post a Comment