Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria.
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria.
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja Nigeria
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Na Andrew Chale
MBUNIFU
mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki
aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho kubwa la mavazi ya
ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho
hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota
tano ya Sheraton Abuja, usiku wa April 25, huku likiudhuriwa na watu
wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na
balozi anayewaiwakilisha Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.
Akizungumza
na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria, Asia Idarous
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa
kuandaa onyesho hilo maalum, kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye
nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
“Hii
ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika
na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya
ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja
nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema
baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai
kutoka Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria
na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe
hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi
mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho
hilo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda,
Fatma Mwinyi, Salma Maulid na wengine wengi.
“Utanzania
wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha ndani na nje
ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza
tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao
‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
Nigeria
ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa
mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na
mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija na hata Taifa
hilo kuwa juu kiuchumi.
No comments:
Post a Comment