Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 2, 2014

MTANANGE WA TSN v/s MLIMANI TV, TSN WATINGA HATUA YA PILI, MLIMANI TV 'OUT' KWA KUCHEZESHA MAMLUKI


 Mchezaji wa TSN, Abubakar Kombo (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Mlimani Tv, wakati wa mchezo wa Kombe la NSSF kwa Vyombo vya habari uliochezwa jana jioni kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe. 
Katika mchezo huo Mliman Tv walinyang'anywa ushindi baada ya kuchezesha vijana wasiokuwa wafanyakazi 'Mamluki' baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mengi kwa bila. Kwa matokeo hayo sasa TSN imetinga katika hatua ya pili ambapo inatarajia kukipiga na Mwananchi Jumamosi asubuhi.
 Beki wa TSN, Sufianimafoto, akikokota mpira kujaribu kuelekeza mashambulizi langoni mwa wapinzani.
 Kipa wa TSN, Idrisa (kushoto) akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Aidan (kushoto) akikimbia kujaribu kuwahi kukaba nafasi, lakini wapi jamaa wanatoka nduki bwana usipime.
 Beki wa TSN, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mliman Tv. (hawa jamaa wote majina yao hayajulikani) 
 Mtanange ukiendelea....
 Dogo akimfinya mtu mzima.......
 Mapumziko, wachezaji wa TSN wakijadiliana wakati wa mapumziko.
 ''Pale mbele jamaa wanacheza wao tu, vipi imekuwaje??????''
 Aliyevaa Suluali ya Khaki na Shati la Draft ndiyo hasa aliyestahili kucheza lakini kutokana na kikosi chao kuwa kamili kwa kusheheni 'Mamluki', jamaa alikosa namba na kuamua kuja kama anaenda ofisini na hapa anaonekana akiwapongeza wachezaji wake.
Akiendelea kuwapongeza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...