Maandamano
ya kuelekea katika uwanja wa Taifa Mjini Kahama yaliojumuisha Timu 26
tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya Mapesya Cup
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama benson Mpesya akisamiana na Wachezaji wa Timu ya
Ngaya FC katika uzinduzi wa mashindani ya Mpesya CUP yalionza juzi
Wilayani Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akifungua mashindani ya Mpesya Cup yatakayosaidia kupata Timu ya Wilaya ya Kahama
Baadhi ya Tumu zilizshirikia katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya Mpesya CUP
Wachezaji wa Timu mbalimbali wakiwa katika maandamno
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja nae alikuwa mmoja kati ya Viongozi walishiriki katika maandamano hayo
Mkuu wa Wilaya Kahama Benson Mpesya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakiwa katika maandamano
Na Wiliama Bundala matukiodaima.com kanda ya Ziwa
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imesema
kuwa haitawatupa Vijana hasa katika masuala mazima ya michezo kwa lengo la
kuinua uchumi wa Wilayani hii sambamba na kupata timu itakayoshiriki ligi kuu
kwa miaka ya mbele.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mpesya aliyasema hayo
wakati akifungua mashindani ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpesya cup ambayo
yanashirikisha jumla ya timu 26 za Wilaya ya Kahama.
Mpesya alisema kuwa haiwezekani Wilaya ya Kahama
pamoja na kuwa rasilimali nyingi ikiwemo wawekezaji katika sekta za migodi na
Tumbaku wapo lakini Wilayah ii inakosa timu inayishiriki ligi kuu hapa nchini.
Aidha alisema kuwa lengo la mashindano ya Mpesya cup
ni kukuza vipaji kwa Vijana wa Wilaya ya Kahama sambamba na kutafuta wachezaji
ambao wataunda timu ya kombaini ya Wilaya ya Kahama ambayo itashiriki katika
mashindano mbalimbali.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama aliendelea kusema kuwa
mpira ni starehe na inakuza akili na kungeza kuwa kwa sasa pia ni ajira hali
ambayo itawafanya wachezaji kufanya michezo kama sehemu yao ya kujipatia
kipato.
“ Kwa sasa tumedharia Wilaya ya Kahama lazima tupate
timu itakayocheza ligi kuu kwa hali tunayo na Rasilimali tunazo na wachezaji
tumieni michezo katika katika kuonyesha viapaji vipaji vyenu ulionavyo”,
Alisema Mkuu wa Wilaya ya kahama Benson Mpesya.
Pia aliwataka wachezaji kutumia michezo kama sehemu
ya kujenga urafiki na mahusiano mazuri
na kutoa onyo kwa waamuzi mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo
hiyo kwa kufuata sheria 17 za soka.
Katika michezo hiyo hiyo ya Mpesya cup mshindi wa
kwanza atapata zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na seti moja ya jezi,
kikombe na mpira mmoja wakati wa pili
atapa kiasi cha shilingi 500,000 pamoja na seti moja ya jezi na mpira .
Michuano hiyo tayari imeanza juzi kwa mechi moja
katika timu ya Ngaya FC na Ambassador na kumalizika kwa matokeo ya timu ya
Ambassador kuinfunga timu ya Ngaya FC kwa jumla ya mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment