Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 13, 2014

TBL YAZINDUA RASMI MASHINDANO YA CASTLE LAGER PERFECT 6, JIJINI DAR MSHINDI KUWASHUHUDIA BARCELONA LIVE CAMP NOU


Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindao ya Castle Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi jijini. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo.
Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika jana kwenye ufukwe wa Mbalamwezi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah.
************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Dar
Timu ya Soka ya Puyo chini ya Nahodha wake Majuto Omary jana jioni iliibuka kidedea katika mashindao ya Castle Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi jijini.

Mashindano hayo ambayo yalijumuisha timu sita za waandishi wa habari za Michezo yamezinduliwa juzi ambapo timu hiyo ya Puyo ambayo ilikuwa na wachezaji wengi wazee, imetinga moja kwa moja kwenye fainali za Taifa zitakazofanyika mwishoni mwa mwezi Julai.

Puyo ilinyakua zawadi ya Kombe na Medali kutoka kwa wadhamini wa mashindano ya hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle baada ya kuzisambaratisha timu za Xavi, Mess, Neymer na Masherano.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo alisema mashindano hayo yatashirika wachezaji wa baa mbali mbali ambao wanatumia kinywaji cha Castle na kwamba yataanza kwa ngazi ya baa, Kanda hadi Taifa ambapo timu sita zitapatikana na kuungana na ile ya Taswa ambapo zitacheza fainali na timu itakayoibuka kidedea katika shindano hilo la Perfect Six watapata fursa ya kutembelea uwanja wa Camp Nou na kujionea timu ya FC Barcelona ikicheza katika ziara ambayo itagharamiwa na Castle.

"Shindano hili litadumu kwa miezi mitano, litafanyika nchi nzima, ambapo timu mbali mbali katika Kanda saba zitasajiliwa na kucheza katika hatua ya mtoano kenye maeneo mbali mbali ambayo yatachaguliwa na kutangazwa mapema.

"Kila kanda itatoa timu moja na kufanya kuwa jumla ya timu saba ambazo zitawakilisha kanda hizo huku timu ya nane ikiwa ni Puyo ambayo inaundwa na waandishi wa habari, timu hizo zitachuana kwa mtoano kwenye robo fainali, nusu fainali na hatimaye fainali.

Naye Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah akifafanua zaidi alisema "Sio kwa wachezaji tu kutakuwa pia na droo maalum kwa wanywaji wa Castle na wateja wawili nao watapata fursa ya kwenda Hispania kujionea Barcelona inavyocheza  na pia kila wiki kuna zawadi ya Sh100,000 itatolewa kwa washindi sita.

Hata hivyo Fimbo alionya kuwa shindano hilo la Perfect Six halitawahusisha wachezaji wa zamani ambao wameshachezea timu mbali mbali za Ligi Kuu, na kwamba litahusisha wale tu ambao hawajawahi kucheza mpira kabisa katika ngazi yoyote inayotambulika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...