Amekua
mmiliki wa vichwa vya habari kutokana na ripoti mbalimbali ambazo
zimekua zikimnukuu kwa kudai kutoutaka muungano lakini leo April 15 2014
amezungumza kwenye maonyesho ya miaka 50 ya muungano ya kuzitoa hizi
kauli zifuatazo.
1.
‘Pamoja na milima na mabonde, muungano huu umedumu miaka 50, nchi
nyingine zilishindwa, lazima tufanye tathmini hasa ya muungano wetu,
lazima vijana waelimishwe vp muungano uliundwa, tulianzia vipi’
2.‘Ukitaka
upate maenedeleo, yatambue mafanikio yako lakini pia usisahau matatizo
yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika Tanzania kama kuna
watu hawataki muungano, na kama wapo ni wachache, muungano uendelee ndio
la msingi’
3.
‘Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio dhambi hata kidogo kwa
sababu hatuwezi wote kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali moja
wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka tatu na serikali ya mkataba
wasikilizwe pia’
4.
‘Wako wanaoamini kwamba matatizo ya muungano yako kwenye muundo,
tuwasikilize wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na Tanganyika maendeleo
ya sehemu zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize, changamoto
kwetu ni vipi tutakua na muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo ya
haraka, mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5.
‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja, tujiepushe na kikundi chochote
kuona wao wana haki zaidi, Watanzania wote sawa, wajumbe wa bunge maalum
waangalie maslahi ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua dola
huru na kuungana kwa hiari’
6.
‘Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro, kero iwe ni historia… hili
swala lisiwepo tena, tusiende kwenye maamuzi ya harahaharaka tukasema
serikali mbili au tatu bila kuangalia athari zake, katiba ya Znz inasema
ni miongoni mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano inasema Tz ni nchi
moja, huo ni mgogoro’
7.
‘Nadhani Warioba walivyopendekezwa waliona hisia za Znz zilivyo,
tunataka katiba itakayotambua usawa wa nchi mbili, hakuwezi kuwa na
katiba ambayo itamridhisha kila mtu lakini angalau wengi wao waridhike’
CHANZO NI MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment