Steve Nyerere akifafanua jambo |
Wadau wa filamu wakifuatilia mjadala huo kwa umakini |
Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisoo akifuatilia jambo katika mjadala huo, |
WASANII
na filamu wametakiwa kutengeneza filamu zenye kuendana na maadhi ya
kitanzania ikiwa pamoja na kutangaza uzuri wa nchi ya Tanzania.
Pia wametakiwa kutumia DVD na CD zenye ubora unaoweza kuhifadhi kwa muda mrefu filamu zao.
Wito
huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga wakati akifungua mkutano
ulioshirikisha wadau wa filamu nchini kwa lengo la kujadili mustakabali
wa fani hiyo.
Katika
mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Taifa, Sihaba aliwataka wadau
hao kujadili kwa kina suala zima la mikataba kandamizi kwa wasanii ikiwa
pamoja na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kutatua kero hiyo.
Sihaba
pia alisema kuwa kupitia kikao hicho ndio kitatoa mwanga kwa serikali
kupitia Wizara yake kutafuta mwafaka wa kero zao mbalimbali.
"Kupitia
mjadala huu ndio serikali itajua mengi mfano mzuri ni suala zima la bei
elekezi inayotakiwa kutumiwa katika kuuza filamu zenu, sasa basi mtumie
vema mijadala kama hii kutupatia mwanga wa nini tunachotakiwa kufanya
ili kuwasaidia"alisema Sihaba.
Katika
kikao hicho cha kujadili mustakabali wa soko la filamu mwenyekiti wa
Bongo Movie Steven Nyerere alisema kuwa mbali na changamoto mbalimbali
zinazoikabili tasnia hiyo zipo ambazo zingepaswa kuwa zimeshatatuliwa
hadi sasa.
Alisema
kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia suala zima la uharamia
katika kazi za filamu huku kukiwa hadi sasa hakuna hatua madhubuti
inayochukuliwa kukabiliana na hali hiyo.
Alisema kuwa hiyo inaathiri mustakabali mzima wa filamu hapa nchini kwa kuwa wasambazaji wanashindwa kufanya kazi zao kwa faida.
Pia aliitaka serikali kuhakikisha kuwa inawawezesha wasanii kuigiza filamu zao hata katika maeneo nyeti kama vituo vya polisi.
"Ndio
maana filamu zetu yabi ni pale pale kama msanii akiigiza chumbani
akitoka yupo sebuleni au mtaani au baa yani kunakuwa hakuna utamu wa
uigizaji wenyewe sasa kwa nini tusiigize hata katika vituo vya polis kwa
mfano"alihoji Nyerere.
No comments:
Post a Comment