Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 7, 2014

MATUMLA AAPA KUMSAMBARATISHA MIYEYUSHO


   Bondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 -26-04-2014
              ------------------------------
--------------------
BONDIA Mohamed Matumla 'Snake JR' ameapa kuwa bondia Francis Miyeyusho 'Chichi Mawe' hatotoka salama siku ya mpambano wao wa aprili 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam
akizungumza kuhusu pambano hilo linalosubiliwa kwa hamu na watanzania wengi kwa ujumla pamoja na nchi za jirani Mohamed Matumla amesema amekuwa akitafuta kwa muda mrefu sana miyeyusho lakini ajapatikana madhamini

amaye angeweza kudhamini mpambano huo ila kwa sasa namshukulu promota Ally Mwazoa kutoka tanga kwa kujitokeza kudhamini mpambano huo litakalokuwa chini ya TPBO na rais wake Yassin Abdallah 'Ustadhi'

ambaye mara nyingi amekuwa akiwasaidia vijana chipkizi kuibua vipaji vyao na kujulikana katika masumbwi nchini
nimemjua Miyeyusho kwa kuangalia mapambano yake mungi tu aliyopigana na nimemuona ana madhala yoyote hivyo nina uwezo wa kumkabili kikamilifu
mana hata mabondia aliocheza nao ni wachovu tu ambao ata mimi nishawai kukutana nao na kuwachapa vibaya sana
hata hivyo yeye anachotambia ni kumpiga baba yangu mdogo  Mbwana Matumla mara moja wakati yeye kapigwa marambili huku wakiwa wamecheza mara tatu katika michezo yao huku mimi nikimpiga mdogo wake Doi Miyeyusho  kama mwizi mara mbili mfululizo ambapo nimecheza nae mara mbili na mara zote nimekuwa nikimpiga kwa K,O ya raundi ya pili kipigo ambacho nilikuwa nikimpiga bila huruma hivyo inawezekana anataka kulipiza kisasi cha kumpiga mdogo wake ata hivyo atadhalilika kwa kipigo nitakacho mpatia

nina endelea na mazoezi yangu vizuri chini ya mwalimu wang Baba yangu Rashidi Matumla na nina haidi nitampiga miyeyusho katika hali ambayo watu awatahamini kipondo nitakacho mpatia mana nitambana kila kona najua ana ufundi kama niliokuwa nao mie mimi ni zaidi

mana nina kipaji alisia zaidi kutoka kwa baba yangu mzazi ninaloomba kwa wapenzi wangu wote na wakazi wa Temeke wajitokeze kwa wingi waje kuona siku hiyo nikimaliza rasmi ufalme wa Miyeyusho katika masumbwi pia kuona maajabu na mageuzi mapya katika masumbwi ya kulipwa

 

nina watangazia rasmi  watanzania wote kuwa hii ni vita ya kisasi na naapa miyeyusho awezi kufuta uteja kwa kuwa nimemchapa mdogo wake nitaendeleza kichapo tu kulinda heshima ya familia ya ukoo wa kina matumla

nawaomba TPBO walete daktari ambaye atatupima mkojo kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu hili ni lifanyike kwani hatuwezi kuwa na mabigwa wanaotumia nguvu za bandia
wakatambulika Duniani kuwa ni mabingwa alimaliza kusema Sneke JR ambaye anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Miyeyusho April 26 katika ukumbi wa PAT Sabasaba Dar es salaam 
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...