Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 20, 2014

MAKOMBE YA DUNIA FEKI 1000 YAKAMATWA NCHINI CHINA



article-2606822-1D27D1F700000578-902_634x420 

Maofisa wa kuzuia bidhaa zisizo na hati miliki nchini China wamekamata makombe feki  ya kombe la dunia zaidi ya 1,000 katika ghala ya kampuni moja kubwa ya utengenezaji na usafirishaji wa bidhaa
Just like the real thing? The mementos found in Yiwu city were due to be exported to Libya 
Kama makombe halisi?, mzigo huu umekamatwa katika mji wa Yiwu tayari kwa safari ya kwenda nchini Libya
Golden: With a group including Uruguay and Italy, the fakes could have been England's best shot at glory 
NDOTO ya mashabiki wa timu ya Taifa ya England `Simba watatu` ni kunyanyua kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
 Lakini suala hili limechukua sura mpya na shukurani za dhati ziwaendee viongozi wa desturi wa China waliofanikisha kukamata mzigo feki.
 Nchi ya China imekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya elfu moja ( 1,000) katika ghala ya kampuni moja kubwa ya usafirishaji nchini humo.
 Makombe hayo feki 1, 020  ya kombe la dunia yamekamatwa katika mji wa Yiwu, jimbo la Zhejiang, ambalo ni moja ya miji mikubwa ya usafirishaji wa bidhaa duniani.
 Makombe hayo feki kwa asilimia kubwa yanafanana na makombe halisi ya FIFA na yalikuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Libya.
 Mkurugenzi wa desturi wa China mwenye mamlaka ya kuzuia nyara zisizohalali alianzisha kampeni mwezi huu wa nne ili kukamata bidhaa zote feki zilizotengenezwa kuelekea kombe la dunia bila kuwa na hati miliki.
Kombe la dunia nchini Brazil linatarajia kuwa na biashara kubwa, na China wameshakamati dili hili na viwanda vyake vimetengeneza bidhaa nyingi za kombe hilo, lakini kuna wajanja wachache wanaotaka kujinufaisha bila ya hati miliki.
 Nahodha wa England Steven Gerrard  ana matumaini ya kubeba kombe halisi mwaka huu nchini Brazil ambapo wapo kundi moja na mataifa ya Italia, Costa Rica na Uruguay.Source DJ Sek BLOG

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...