Mmoja
wa washiriki wa Shindano la kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania,
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) Bw Stephen Mapunda
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza
kwa zoezi la usaili katika shindano la TMT.
Baadhi
ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya Kushiriki katika shindano la
kusaka vipaji vya uigizaji wakiwa katika mstari tayari kwa kupewa fomu
ya usaili ili kuweza kushiriki kwenye shindano la TMT.
Baadhi
ya washiriki waliofika katika ukumbi wa African Dream kwaajili ya
usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya shindano hilo ambalo
kwasasa linaendelea Katika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma.
Kundi
la kwanza likiwa tayari kwaajili ya kupewa namba za ushiriki mara baada
ya kumaliza zoezi zima la kujaza fomu za ushiriki katika shindano la
kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents
linaloendelea kufanyika Mkoani Dodoma leo ikiwa inawakilisha Kanda ya
Kati.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.
Shindano
la Tanzania Movie Talents leo limeingia siku ya pili ya usaili mkoani
Dodoma, Kanda ya Kati ikiwa na washiriki waliojitokeza zaidi ya 600.
Shindano hili limeibua hisia za Watu wengi kutokana na Umahiri wake na
kuwa shindano la kwanza kutokea Afrika Mashariki na Kati huku maandalizi
yake yakiwa yamefanyika kwa umakini wa hali ya juu huku Majaji wa
Shindano hilo wakitokea kuwa Vivutio vikubwa kwa washiriki hao kutokana
na jinsi wanavyotoa Uamuzi.
Washiriki
zaidi ya 600 wameweza kujitokeza kushiriki shindano hili ili kuweza
kuonyesha vipaji vyao na mpaka sasa zoezi hili limeingia siku ya pili
ambapo timu ya TMT imeendelea kusaili vijana waliojitokeza.
Safari
ya Mchujo wa shindano hili kwa kanda ya kati ambapo shindano hili
linafanyika mkoani Dodoma utaanza kufanyika kesho Jumatatu ili kuweza
kupata washindi watatu bora ambao kila mmoja atajiondokea na Kitita cha
Shilingi laki tano (500,000) kwa kila mshindi na baadae kujiunga na
washindi wengine wa kanda zilizobakia Kwaajili ya fainali kubwa
itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na kupelekea Mshindi kujinyakulia
zawadi kubwa kabisa ya Kitita cha pesa za Kitanzania Milioni 50
(50,000,000/=) na vilevile washindi kumi bora katika fainali hiyo
watakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions na watafanya
kazi ya pamoja na hatimaye kazi yao kuweza kuuzwa nchini nzima na wao
kunufaika na kazi hiyo.
Shindano
hili linaloendelea kufanyika mkoani Dodoma linatarajiwa kumalizika
mnamo Jumanne ya 15 April 2014 na siku hiyohiyo Washindi watatu
watatangazwa.
Baada
ya shindano hili kumalizika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, shindano
litaelekea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya kwaajili ya vijana
kuweza kuitumia fursa hii kwaajili ya kuonyesha Uwezo na vipaji vyao
katika Kuigiza.
Katika
Shindano hili vijana wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuitumia
fursa hii na hatimaye kuweza kuonyesha vipaji vyao kwa maana huu ndio
muda wao.
Hakuna viingilio katika shindano hili na fomu zinapatikana bila gharama yoyote ile.
No comments:
Post a Comment