Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia
tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku
mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi
zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba
zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake
ni sh. 7,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya
chungwa, sh. 20,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tayari
tiketi zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya;
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu),
Buguruni Shell, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo
OilCom, Dar Live Mbagala na Uwanja wa Taifa.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Oljoro JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta
Amri Abeid, Arusha) na Coastal Union na Kagera Sugar (Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga).
No comments:
Post a Comment