Na Andrew Chale
KUNDI
la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan Safaa (Malindi), wanatarajiwa
kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wa burudani wakiwemo mashabiki wa
soka wa Azam Fc waliokwisha chukua ubingwa Ligi kuu Tanzania Bara,
kwenye onyesho maalumu la ‘Usiku wa Mwambao Asilia’, ndani ya ukumbi wa
Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Aprili 19.
Akizungumza
jijini Dar es salaam, Mratibu wa onyesho hilo la pamoja Dar Modern na
Nadd Ikhwan Safaa (Malindi ya Zanzibar), Bakari Hassan alisema hilo la
Usiku wa Mwambao Asilia, litaenda sambamba na kuwapongeza mashabiki wa
soka wa Azam Fc waliotwaa ubingwa huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara
ya kwanza 2013/2014.
“Usiku
wa Mwambao asilia, Aprili 19, pale Travertine utakuwa na shamrashamra
mbali mbali ikiwemo za kuwapongeza Azam na mashabiki wao watakaofika
kwenye onyesho hilo maalum” alisema Bakari.
Kwa
upande wake, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema usiku
huo pia utakuwa ni maalum ikiwemo pia kuwakutanisha magwiji wakongwe wa
muziki wa taarabu nchini, ambao wataimba nyimbo za zamani na za sasa.
“Kwa
kiingilio cha sh 10,000 tu, usiku huo utapambwa na ‘surprise’,
mbalimbali kwa wadau kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga
picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo” alisema Asia
Idarous.
Aidha,
Asia, alisema tayari tiketi za onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa sehemu
mbalimbali ikiwemo duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni
na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia
limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions nawww.nakshi255.com
No comments:
Post a Comment