Na Andrew Chale
WAPENZI
wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini Jumapili hii ya Aprili 6,
wanatarajiwa kupata burudani safi na ya aina yake kutoka kundi la
Spice Modern Taarab, ndani ya ukumbi wa Regency Park Hotel,m iliyopo
Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, ambao ni
miongoni mwa wadhamini wa onyesho hilo, kwa kushirikiana na Regency
Hotel, amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi kuufurahia kukumbushiana
enzi za muziki wa mwambao wa taarab.
Asia
Idarous alisema onyesho hilo pia litakuwa ni la kila siku ya Jumapili
katika ukumbi huo ndani ya hoteli hiyo ya Regency, eneo lenye mazingira
safi na upepo mwanana huku kiingilio kikiwa cha kawaida cha sh 5,000.
“Kila
Jumapili Spice Taarab watakuwa wakitoa burudani ya nyimbo za mwambao
hasa zile zilizokuwa zikipendwa, kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita
usiku,” alisema Asia Idarous.
Asia
Idarous pia alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zimekuwa gumzo kipindi
hicho ni pamoja na ‘Pendo kitu cha hiari’, ‘Dunia ina fisadi’, ‘Kasha’
na nyingine nyingi. Aidha aliongeza kuwa Regency Park itakuwa ni kiota
cha burudani ya miziki hiyo ya zamani huku usiku huo ukiwa unajulikana
kama ‘OLD IS GOLD’ na watu mbalimbali wakitarajiwa kukutana hapo na
kubadilishana ya zamani
Kwa
upande wa Wadhamini katika usiku huo wa taarabu asilia ni pamoja na
Times FM, Regency Park Hotel na Fabak Fashions, Pia alitoa wito kwa
wadau wengine watakao kuwa tayari kudhamini kujitokeza kuchangamkia
fursa hiyo kwa kuwasiliana na namba .0784263363 au0713263363
No comments:
Post a Comment