Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 29, 2015

MAPATO YA TAZARA COMPUTER TRAIN YAONGEZEKA KWA KASI


 
 
KAMPUNI ya Selcom Tanzania imesema kwa kushirikiana na Tazara imefanikiwa kuongeza mapato ya fedha kwa mfumo wa ukatisha tiketi ulioanza kutumiwa na shirika la reli la Tazara.

Akizungumza na mwandishi  wa gazeti hili, Bw. Juma Mgori,  ambaye in Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya Selcom Tanzania, alisema  kupitia vifaa vyao vya kukata tiketi (POS), wananchi wameondolewa adha kubwa waliyokuwa wakiipata wakati wa kukata tiketi katika shirika reli la Tazara.

Alisema kuwa, kutokana na mpango huo,  TAZARA imefanikiwa kuongeza mapato kwa abiria kukatiwa tiketi kwa mfumo wa mashibe hizo.

Mfumo huo ni rahisi na bora zaidi na hivi karibuni kampuni ya Selcom inatarajia kuzindua kadi zake mpya za malipo zijulikanazo kama SELCOM PAYPOINT CARD ambazo mbali na malipo mbalimbali na uwezo wa kutuma Pesa kwenye mitandao yote.

 Kadi hizo zinaweza kuwa njia sahihi kwenye njia za usafiri kama treni, mabasi ya mikoani na hata daladala.

Bw. Mgori alisema kuwa, kadi hizo ni salama na zenye uwezo mkubwa zikiwa zimethibitishwa na kuidhinishwa katika viwango vya nchini na hata vya kimataifa.

"Tunajivunia ubunifu wetu huu ambao unafanyika hapa nyumbani na kampuni ya kizawa na wataalamu wazawa. Ikumbukwe pia kadi hizi hivi sasa zinatumika na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa wale wastaafu kutoa Pesa zao na ziko kwenye majaribio.

SUPER D AHAMASISHA UWANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA


 
 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiweka alama za vidole wakati wa uhandikishwaji wa vitambulisho vya kupigia kura iliyokuwa ikifanyika katika kitongoji cha Buguru Dar es alaam kulia ni muhandikishaji wa kituo hicho Karim Ibrahimu
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiweka alama za vidole wakati wa uhandikishwaji wa vitambulisho vya kupigia kura iliyokuwa ikifanyika katika kitongoji cha Buguru Dar es alaam kulia ni muhandikishaji wa kituo hicho Karim Ibrahimu


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchinini Rajabu Mhamila  Super D akitia saini kitambulisho chake kabla akijatoka kwa karani wa Karim Ibrahimu

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' askiangalia picha yake kabla akijatengenezwa kitambulisho kwa karani Karim Ibrahimu ilikuwa mpiga picha anapopigwa picha na mtu mwingine

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiweka akionesha kitambulisho chake
Rajabu Mhamila akiwa ametulia

Thursday, July 23, 2015

NJAMA ZA MAKABURU KUMG'OA MKURUGENZI WA KONYAGI MGWASSA ZAGUNDULIKA



 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), maarufu kwa jina la Konyagi . David Mgwassa Kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) Jijini Dar es Salaam.Mwandishi Wetu

MKAKATI wa kumng'oa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi (TDL) David Mgwassa umebainika kutokana na kuwepo kwa njama zinazoendeshwa kwa siri na makaburu.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kiongozi huyo amekuwa akipigwa vita kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mafanikio yanayopatikana chini ya uongozi wake.

Makaburu hao wamekuwa wakifanya njama mbalimbali za kumng'oa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutaka kushika wadhifa wa mkurugenzi huyo kwa kutoa taarifa ambazo si za kweli kwa uongozi wa ngazi za juu nchini Afrika Kusini na Uingereza.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kukabidhi ofisi ifikapo Julai 30, mwaka huu.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa tayari taarifa za kuondolewa kwa kiongozi huyo zimezagaa katika viwanda vya TDL na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) pia tangazo la kumbadilisha limetolewa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kutangaza Kenya na Uganga.

Kutokana na taarifa hizo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TDL wameazimia kugoma ili kushinikiza mkurugenzi huyo kuendelea na madaraka yake.

"Tumesikia taarifa kuwa mkurugenzi wetu anaondolewa madarakani kwani tumeshangazwa sana kutokana na kuishi naye vizuri na kupatikana kwa mafanikio mengi tangu ashike wadhifa huo na pia ameboresha maisha yetu kwa kutuongezea mishahara," alisema mfanyakazi mmoja ambaye hakutaja jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa wafanyakazi.

Hata hivyo kuna taarifa kuwa Bw. Michael Benjamin anatarajia kushika wadhifa wa Bw. Mgwassa.

Mtandao huu ulimtafuta Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Steve Kilindo ili kuzungumzia taarifa hilo alikiri kuwepo kwa mabadiliko hayo lakini hana taarifa zaidi kuhusiana na sakata hilo.

"Kweli kuna mabadiliko hayo ya uongozi lakini taarifa za ndani sina," alisema.
                         Mike Benjamin kutoka Afrika Kusini anayetarajia kurithi cheo hicho

Friday, July 17, 2015

MABONDIA WA KIKE KUZIDUNDA KESHO

Promota Stamili Mmtengwa katikati akiwainuwa juu mabondia Mwanne Haji kushoto na Lulu Kayage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika sikukuu ya Iddi Mosi katika ukumbi wa Frends Corner  Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Mmwanne Haji kushoto na Lulu Kayage wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Iddi Mosi Katika ukumbi wa Frends Ccorner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Lulu Kayage akipimwa na Ddokta Michael Madadidi kwa ajili ya mpambano wake na mwanne Haji

Promota Stamili Mmtengwa katikati akiwainuwa juu mabondia Habibu Pengo kushoto na Yonas Segu

Bondia Mwanne Hhaji akipimwa Afya na Dokta Mmixchael Midadi

Bondia Lulu Kayage akipimwa na Ddokta Michael Madadidi kwa ajili ya mpambano wake na mwanne Haji

Tuesday, July 14, 2015

NHIF YAIPIGA TAFU TIMBERLAND JOGGING YA YOMBO KILAKALA

Mlezi wa kikundi cha Timberland Jogging cha yombo Kilakala  Carren Mgonja akiwazungumza na maofisa wa Mfuko wa Afya ya Jamii NHIF walipowatembelea makao yao makuu 

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Timberland Jogging wakisoma vipeperushi vya Mfuko wa Afya ya Jamii NHIF 

Mlezi wa kikundi cha Timberland Jogging cha yombo Kilakala  Carren Mgonja kushoto akipokea fulana kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii NHIF .Eugen Mikongoti wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Samir Choray na maofisa wa NHIF

 Mlezi wa kikundi cha Timberland Jogging cha yombo Kilakala  Carren Mgonja kushoto akipokea msaada wa fulana kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii NHIF .Eugen Mikongoti wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Samir Choray na maofisa wa NHIF
Makao makuu ya kikundi cha Timberland Jogging wanachama wakiwa na maofisa wa NHIF baada ya kugawa msaada wa fulana pamoja na ahadi ya kufanya kazi p-amoja na kikundi hicho kilichopo Yombo Kilakala

Monday, July 13, 2015

MABONDIA WA KIKE KUMALIZA UBISHI SIKU YA IDDI MOSI KATIKA UKUMBI WA FRENDS CORNER MANZESE DAR





Na Mwandishi Wetu

 MABONDIA wa kike kupanda uringoni siku ya Iddi Mosi katika ukumbi wa frends corner Manzese Dar es Salaam mambondia hawo ni Lulu Kayage ambaye atavaana na Mwanne Haji katika mpambano wao wa raundi sita uzito wa kg 49 

Mratibu wa mpambano uho Dikumbwaya Mtengwa siku hiyo pia kutakuwa na ngumi kazi za wanaume wa shoka alisema bondia

Yonas Segu atapambana na Habibu Pengo mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63 na  Nassibu Ramadhani Kudura Omar mpambano wa kg 53 raundi sita wakati Shadrack Juma atakabiliana na Bakari Ostadhi 
mbali na mipambano hiyo ya ngumi pia kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo ambatana na sherehe ya sikukuu ya Iddi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

BONDIA MOHAMED MATUMLA KUMVAA KOBA DONATI IDI PILI BAGAMOYO



Na Mwandishi Wetu

BONDIA Mohamed Matumla anatalajia kupanda tena uringoni siku ya Idi pili katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani kupambana na Koba Nodat katika uzito wa KG 57 mpambano wa raundi sita Matmla anapambana mpambano uho baada ya mpambano wake wa mwisho kumtwanga Mchina kwa point

mratibu na promota wa mpambano uho Muhsin Sharif amesema amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi litawakutanisha bondia Iddi Pialali kutoka Kiwangwa Bagamoyo na Mesharck Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano wa raundi nane kg 66 wakati bondia machachari katika tasnia ya mchezo wa masumbwi nchini Vicent Mbilinyi atavaana na Khalidi Hongo mpambano wa raundi nne wakati Twalibu Tuwa atavaana na Sudi Sudi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

YANGA KUANIKA SILAHA ZAKE MBELE YA WAZIRI PINDA




http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/Mizengo-Pinda1.jpgSTRAIKA Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe alitarajiwa kutua nchini jioni ya leo na ilitarajiwa jioni ya kesho angeishuhudia Yanga inayotaka kumsajili ikitambulisha nyota wake wapya katika pambano dhidi ya Sc Villa ya Uganda.
Hata hivyo mchezaji huyo imeshindikana kutua leo, lakini hakuna kilichoharibika kwani Yanga itatambulisha nyota wake wote mbele ya Waziri Mkuu na Mtangaza Nia ya Urais, Mhe. Mizengo Pinda. Waziri Pinda atakuwepo katika pambano hilo ili kubariki silaha hizo mpya za Jangwani wakati wa mchezo huo maalum wa kuchangisha fedha za Ujenzi wa Majengo ya Watoto Wanaoisha katika Mazingira Magumu.
MKurugenzi wa asasi wa Nyumbani Kwanza, Mossy Magere aliiambia MICHARAZO MITUPU kuwa, Yanga itavaana na SC Villa ambapo pia kutakuwa na burudani ya kutosha kwa watakaohudhuria.
Mossy alisema kuwa, Waziri Pinda ndiye mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo Yanga watalitumia kutambulisha nyota wake wapya na kusindikizwa na burudani ya muziki toka kwa kundi la Yamoto Band.
"Maandalizi yamekamilika na kwamba wageni mbalimbali tumewaalika, ila Waziri Pinda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi na atabariki kikosi hicho cha kocha Hans Pluijm," alisema Mosi.
Mosi alisema kuwa SC Villa walitua juzi jioni wakiwa na kikosi cha wachezaji 18 na viongozi watano na kwamba jana walipasha misuli kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya leo kuivaa Yanga.
Yanga ambao imetoka kuichapa Friends Rangers kwa mabao 3-2 katika mechi ya mazoezi, inauchukuliwa kwa uzito mkubwa mchezo huo wa leo kwani ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wao wa michuano ya Kagame na kocha atataka kupima uwezo wa wachezaji wao mbele ya Villa.
Baadhi ya wachezaji wapya wa Yanga ambao watakuwa majaribuni ni Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na kipa Benedict Tinocco kwani Mwinyi Haji Ngwali na Deus Kaseke wapo kambi ya Taifa Stars kujiandaa na pambano la marudiano la kuwania Chan dhidi ya Uganda The Cranes.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alinukuliwa juzi kuwa, huenda akawashtukiza mashabiki wa klabu hiyo katika mchezo huo wa kesho, bila kufafanua lakini imebainika ni kwamba Donald Ngoma alipangwa kuwepo uwanjani kuwashuhudia wenzake kwani angetua nchini ili kumalizana na klabu hiyo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...