Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 29, 2015

MAPATO YA TAZARA COMPUTER TRAIN YAONGEZEKA KWA KASI


 
 
KAMPUNI ya Selcom Tanzania imesema kwa kushirikiana na Tazara imefanikiwa kuongeza mapato ya fedha kwa mfumo wa ukatisha tiketi ulioanza kutumiwa na shirika la reli la Tazara.

Akizungumza na mwandishi  wa gazeti hili, Bw. Juma Mgori,  ambaye in Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya Selcom Tanzania, alisema  kupitia vifaa vyao vya kukata tiketi (POS), wananchi wameondolewa adha kubwa waliyokuwa wakiipata wakati wa kukata tiketi katika shirika reli la Tazara.

Alisema kuwa, kutokana na mpango huo,  TAZARA imefanikiwa kuongeza mapato kwa abiria kukatiwa tiketi kwa mfumo wa mashibe hizo.

Mfumo huo ni rahisi na bora zaidi na hivi karibuni kampuni ya Selcom inatarajia kuzindua kadi zake mpya za malipo zijulikanazo kama SELCOM PAYPOINT CARD ambazo mbali na malipo mbalimbali na uwezo wa kutuma Pesa kwenye mitandao yote.

 Kadi hizo zinaweza kuwa njia sahihi kwenye njia za usafiri kama treni, mabasi ya mikoani na hata daladala.

Bw. Mgori alisema kuwa, kadi hizo ni salama na zenye uwezo mkubwa zikiwa zimethibitishwa na kuidhinishwa katika viwango vya nchini na hata vya kimataifa.

"Tunajivunia ubunifu wetu huu ambao unafanyika hapa nyumbani na kampuni ya kizawa na wataalamu wazawa. Ikumbukwe pia kadi hizi hivi sasa zinatumika na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa wale wastaafu kutoa Pesa zao na ziko kwenye majaribio.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...