Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 13, 2015

BONDIA MOHAMED MATUMLA KUMVAA KOBA DONATI IDI PILI BAGAMOYONa Mwandishi Wetu

BONDIA Mohamed Matumla anatalajia kupanda tena uringoni siku ya Idi pili katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani kupambana na Koba Nodat katika uzito wa KG 57 mpambano wa raundi sita Matmla anapambana mpambano uho baada ya mpambano wake wa mwisho kumtwanga Mchina kwa point

mratibu na promota wa mpambano uho Muhsin Sharif amesema amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi litawakutanisha bondia Iddi Pialali kutoka Kiwangwa Bagamoyo na Mesharck Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano wa raundi nane kg 66 wakati bondia machachari katika tasnia ya mchezo wa masumbwi nchini Vicent Mbilinyi atavaana na Khalidi Hongo mpambano wa raundi nne wakati Twalibu Tuwa atavaana na Sudi Sudi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...