Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 13, 2015

MABONDIA WA KIKE KUMALIZA UBISHI SIKU YA IDDI MOSI KATIKA UKUMBI WA FRENDS CORNER MANZESE DAR

Na Mwandishi Wetu

 MABONDIA wa kike kupanda uringoni siku ya Iddi Mosi katika ukumbi wa frends corner Manzese Dar es Salaam mambondia hawo ni Lulu Kayage ambaye atavaana na Mwanne Haji katika mpambano wao wa raundi sita uzito wa kg 49 

Mratibu wa mpambano uho Dikumbwaya Mtengwa siku hiyo pia kutakuwa na ngumi kazi za wanaume wa shoka alisema bondia

Yonas Segu atapambana na Habibu Pengo mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63 na  Nassibu Ramadhani Kudura Omar mpambano wa kg 53 raundi sita wakati Shadrack Juma atakabiliana na Bakari Ostadhi 
mbali na mipambano hiyo ya ngumi pia kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo ambatana na sherehe ya sikukuu ya Iddi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...