Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 1, 2016

MABONDIA WAPIMA UZITO NA KUPEWA SEMINA YA UJASILIAMALI ILIYORATIBIWA NA KOCHA SUPER D

MABONDIA WAPIMA UZITO NA KUPEWA SEMINA YA UJASILIAMALI ILIYORATIBIWA NA KOCHA SUPER D

Mabondia Shedrack Ignas kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Ruwanje baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika October 2 katika ukumbi wa white house Bar Kimara Korogwe Picha naSUPER D BOXING NEWS
Mabondia Said Chino akitunishiana misuli na Haidar Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Rojas Masamu baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao kesho katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Dar es Salaam SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Manyi Issa kushoto akitunishiana misuri na Mustafa Doto baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumapili katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Dar es salaam SUPER D BOXING NEWS
Ofisa Vijana Mstaafu  Robert Semkiwa kushoto akitoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana wanamichezo wa mchezo wa ndondi kabla ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa October 2 katika ukumbi wa White House uliopo Kimara Korogwe Dar es salaam mafunzo hayo yalitolewa kwa uratibu wa kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' kwa vijana wa mchezo wa masumbwi

Baadhi ya mabondia makocha na wadau wa mchezo wa masumbwi wakiwa wamesimama kwa ajili ya kufatilia mafunzo hayo
Ofisa Vijana Mstaafu  Robert Semkiwa kushoto akisisitiza jambo


Mkurugenzi wa Tasisi isiyo ya kiserekali YOWEDE  BW. Edwin Mutayoba akisisitiza jambo wakati wa semina ya ujasiliamali kwa wanamichezo wa mchezo wa ndondi

Mwenyekiti wa marefarii wa mchezo wa ngumi Tanzania 'TPBC'  Ally Bakari 'Champion' akifafanua jambo kwa mabondia





Na Mwandishi Wetu

BABONDIA mbalimbali wamepima uzito na kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali kabla ya mpambano wao utakaofanyika siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Bar Kimara Korogwe wamepimwa uzito pamoja na Afya zao


akizungumzia mpambano uho kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye pia ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wamepima uzito pamoja na Faya Zao na kupatiwa semina ya ujasiliamali

Aliwataja baadhi ya mabondia waliopima 
 uzito ni Said Chino atakaezitwanga na haidar Mchanjo uzito wa kg 57 raundi sita wakati Abdallah Ruwanje atavaana na Shedrack Ignas mpambano wa raundi sita la uzito wa kg 63wakati bondia mkongwe kabisa katika mchezo wa masumbwi nchini Mustafa Doto atazipiga na bondia chipkizi Manyi Issa katika uzito wa kg 61 raundi sita

mipambano mingine itawakutanisha mabondia Mohamed Muhunzi atakaepambana na Kassim Ahmad na Hashimu Chisora atazipiga na Rojas Masam uzito wa kg 61 na Julias Jackson atapambana na Emilio Norfat mpambano wa raund 4 uzito wa kg 61  na Ellsame Mbwambo atazipiga na Emanuel Kisawani mpambano wa raundi 4 uzito wa kg 61

mbali ya siku ya leo kesho tena
kutakuwa na elimu ya ujasiliamali kwa vijana wa mchezo wa masumbwi pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujikwamuwa na uchumi 

Mgeni rasmi katika mpambano uho atakuwa 
Humphrey Polepole Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
 
Katika Mchezo huo kutakua na Uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...