Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 29, 2013

NMB YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KIBENKI KARIBU YAKO


 Wateja waBenkiya NMB wakipatamaelekezoyahudumaza JISEVIE kutokakwaOfisawa NMB tawi la NMB House  Edith Mavura.Hudumazitolewazokwawatejawa NMB waliojisajilikutumia NMB Mobile .Hudumainayomuwezeshamtejakupatahudumazakibenkimahalapopotebilakufikakwenyetawi la NMB
 Wateja wa Benkiya NMB wakipata maelekezo yanayohusu maboresho ya huduma ijulikanayo kama JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi .Jisevie inamsaidia mteja wa NMB kupata huduma za kibenki sehemu yoyote atakapokua bila kufika kwenye tawi la NMB.Mteja ataweza kutumia simu yake ya kiganjani na kutembelea Mashine za kutoa fedha ili Kujisevia.
 Ofisawa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi akimwelekeza mteja wa NMB jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB

Ofisa wa  NMB tawi la Loliondo, Lembris Lesion akimwelekeza Mchungaji mstaafu, Ambelikile Mwaisapile jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB.

Na Mwandishi Wetu

NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.

Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.

Huduma zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni pamoja na Huduma ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na huduma ya kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom Mpesa.

“ Mpango huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali wanazoweza kuzipata bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika kuendelea kutoa huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote mteja anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa Mkuu wa Biashara ya Wateja Binafsi.
Wateja ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa katika mpango huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia fedha taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye na akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na kutohitaji kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha kwenye akaunti yako.

Wateja wa NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo bila kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana  NMB Jisavie ambayo itamwezesha mteja wa NMB  kuwa na  NMB Mobile,NMB Pesa Fasta ,POS,NMB ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha  kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye tawi la NMB.

Faida nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango huu wa Jisevie ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa fupi ya matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO, kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua muda wa hewani.

SHIWATA YAONESHA VIPAJI VYA WASANII Star Light Hotel

Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Kaole wakishangilia wakati msanii mwenzao Chuma Selemani 'Bi Hindu' alipokuwa akisalimia na kutoa ujumbe kwa watu waliofika katika tamasha hilo lilili andaliwa na

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)

lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa

Star Light Hotel picha na www.burudan.blogspot.com

Wasanii wa kikundi cha Kaole wakifatilia matukio mbalimbali wakati wa maonesho hayo kutoka kushoto ni Chuma Selemani 'Bi Hindu' Fatma Rajabu' Kidide' Zuhura Adamu 'Mwana mtama' na Rajabu Miromo' Fakh'

picha na www.burudan.blogspot.com

Wasanii wa kikundi cha Kaole wakifatilia matukio mbalimbali wakati wa maonesho hayo kutoka kushoto ni Chuma Selemani 'Bi Hindu' Fatma Rajabu' Kidide'
Mwenyekiti wa

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib kulia akifatilia maonesho hayo

Msanii wa Kikundi cha Kaole Chuma Selemani 'Bi Hindu' akizungumza
Wasanii wa kindi la Tae kwond Vingunguti youth wakifanya mchezo wa Kun Fuu wakati wa onesho hilo
Wapiga ngoma wa kikundi cha Tan hope Group wakifanya vitu vyao
Wasanii wa  ngoma wa kikundi cha Tan hope Group wakicheza wakati wa tamasha hilo tamasha hilo lilili andaliwa na

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)

lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa

Star Light Hotel picha na www.burudan.blogspot.com

Wasanii wa  ngoma wa kikundi cha Tan hope Group wakicheza wakati wa tamasha hilo tamasha hilo lilili andaliwa na

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)

lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa

Star Light Hotel picha na www.burudan.blogspot.com


Sunday, April 28, 2013

SIMBA YAITAFUNA POLISI MOROGORO 2-1

Mrisho Ngassa (kushoto) wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Rogers Gabliel wa Polisi Morogoro wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

 Mashabiki wa Simba wakiwa wachache kwenye jukwaa lao wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo na Polisi Morogoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. (PICHA NA KASSIM MBAROUK)

PINDA AFUNGUA MAONESHO YA AFYA NA USALAMA DUNIANI


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama onyesho la uokoaji kutoka mwokoaji wa mgodi  wa North Mara Gold Mine katika maonyesho ya kuadhimish Siku ya Afya na Usalama Duniani yaliyofanyiaka kwenye uwanaj wa Shikh Amri Abeid jijini Arisha, Aprili 28,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama vifaa vya uokoaji katika banda la maonesho ya kuadhimisha  siku ya Afya na Usalama Duniani kwenye  uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Aprili 28,2013. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea Tuzo

ya Utoaji huduma bora ya   Afya na Usalama kazini

kwa niaba ya  Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa

na Serikali za Mitaa kutoka kw Waziri wa Kazi na

Ajira, Gaundentia Kabaka katika Kilele cha

Maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duaniani

kwenye uwanja wa Shikh Amri Abeid , Arusha Aprili

28, 20113.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DYNA, H.BABA, KITALE NA MASELE WAPAGAWISHA MWANZA UZINDUZI WA ALBAM YA KALA JEREMAYA

Kala Jeremaya kama kawaida yake kutikisa jukwaa ...full mizuka ikiwapanda mashabiki wake leo hii wakati anazindua Album yake ya PASAKA yenye nyimbo kibao 23 ambayo pia amedai kuwa kuifanisha album hiyo ilimchukua muda wake mwingi wa kukaa studio na pia ikiwa ni album moja wapo ya kumjenga kimuziki hapa nchini na nje

Msanii wa kizazi kipya almaarufu kama Dyna akiimba leo Ijumaa hii usiku kwenye Uzinduzi wa Album ya Kala Jeremaya kwenye ukumbi wa raha Jijini Mwanza Villa Park Resort.
Msanii wa kizazi kipya Dyna akiimba nyimbo yake ya Nivute kwako

Djz wakifanya mambo yao jukwaani

Msanii wa kizazi kipya Dyna akiimba huku mashabiki wakipagawa na nyimbo zake 

Shabiki ilibidi apande jukwaani kumsindikiza Dyna

Ilikuwa patashika Villa Park usiku huu Masele amewashika vilivyo mashabiki wake.

Msanii H.Baba akiwa ameshilia album mpya ya Kala Jeremaya usiku huu ambayo imezindulia leo hii rasmi ikiwa na nyimbo

Kala Jeremaya kama kawaida yake kutikisa jukwaa ...full mizuka ikiwapanda mashabiki wake leo hii wakati anazindua Album yake ya PASAKA yenye nyimbo kibao 23 ambayo pia amedai kuwa kuifanisha album hiyo ilimchukua muda wake mwingi wa kukaa studio na pia ikiwa ni album moja wapo ya kumjenga kimuziki hapa nchini na nje

BONANZA LA JOGGING CLUBS MZIMUNI LAFANA LAKUSANYA MAJOGGER KIBAOOOO!

Bila kusahau ndonga, nazo zilikuwepo mapema asubuhi ya leo. Hii ni kwasababu Klabu ya Mzimuni ni Jogging and Sports.

Vikosi vya Jogging vya maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Zanzibar vikiwa mitaani kwaajili ya bonanza maalum lililoandaliwa na Jogging Club ya Mzimuni Magomeni jijini Dar es Salaam. Bonanza hilo ambalo linaendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mzimuni limekusanya karibu Jogging Club 30.
Mazoezi ni afya.
Dawa ya kuachana na ubonge nyanya!
Rika zote wamejumuika pamoja.
Michezo mbalimbali ukiwemo huu wakuchezea baiskeli pia upo!
Wacha banaweee manjonjo tupu! iga uone!
Mashost nao! Ubonge baaaaaaasssss!
Bila kusahau ndonga, nazo zilikuwepo mapema asubuhi ya leo. Hii ni kwasababu Klabu ya Mzimuni ni Jogging and Sports.
Kikosi cha Zanzibar ambacho kilipambana na Mzimuni na kuifunga goli moja bila.
Picha ya pamoja vikosi vyote viwili Mzimuni na Zanzibar.
Kikosi kamili cha Mzimuni.

YANGA YAIVUTIA NGUVU SIMBA KWA KWENDA MAZOEZI YA GYM








PRESHA ya pambano la watani wa jadi imezidi kupanda, baada ya Yanga kujipa mazoezi ya nguvu kusaka pumzi na stamina kabla ya kuwavaa mahasimu wao, Simba, Mei 18 mwaka huu, huku viongozi na timu nzima wakidai kubakiza mechi hiyo kutimiza furaha yao.
Yanga, ambayo tayari imeshatangaza ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, imeona wazi kwamba hakuna sababu ya kubweteka na kusherehekea jambo hilo hadi hapo watakapomalizana na Simba katika mechi hiyo ya kusaka heshima kubwa.
Yanga imebainisha wazi kwamba furaha yao ya ubingwa wa ligi msimu huu haitakamilika kama watashindwa kuifunga Simba, hivyo jambo hilo limeifanya timu hiyo kuingia gym kupiga mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanatunisha misuli, kutafuta stamina na pumzi ya kuhakikisha inawatuliza mahasimu wao kwa dakika zote tisini katika mechi hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wababe hao wa mitaa ya Jangwani wamenyakua ubingwa huo kiulaini, baada ya Azam FC kuambulia sare ya bao 1-1 juzi katika mechi yake dhidi ya Coastal Union, matokeo ambayo yamefanya kusiwepo na timu yoyote inayoweza kufikia pointi za Yanga (56), huku timu hiyo inayonolewa na Mholanzi, Ernie Brandts, ikibakiza mechi mbili.
Lakini, sasa mabingwa hao wapya, Yanga wanadai furaha yao haijakamilika kwa sasa kwa sababu bado hawajawafunga Simba na hilo ndilo linalowafanya nyota wa kikosi hicho pamoja na benchi zima la ufundi kufanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanakuwa fiti katika idara zote.
Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga, alisema wamepokea kwa mikono miwili ubingwa huo wa msimu huu, lakini bado wana kazi moja ya kuhakikisha mashabiki wa timu hiyo wanaendelea kupata furaha kwa kuwafunga watani wao wa jadi, Mei 18 mwaka huu.
Akisema hatua ya kupata ubingwa mapema ni ishara kwamba walikuwa wamejiandaa vyema, huku akiwapongeza wachezaji wake pamoja na benchi zima la ufundi kwa kufanya kazi kwa kujituma na kudai kwamba moto huo utaendelea hadi Mei 18 katika Uwanja wa Taifa.
“Tunaupokea ubingwa kwa furaha, lakini bado tuna kazi nyingine, moja ni kupata ushindi dhidi ya Coastal Union na pili ni kuifunga Simba katika mchezo wa mwisho, hizi ndizo changamoto kubwa zinazotukabili kwa sasa," alisema.
“Kwa hiyo tunawaomba mashabiki na wapenzi wa Yanga kuendelea kuiunga mkono timu hadi mwisho wa msimu kwa sababu tumedhamiria kuwapa raha.”
Katika hatua nyingine, Kocha mkuu wa kikosi hicho, Ernie Brandts ameeleza kuwa pamoja na kupata ubingwa huo wakiwa wamebakisha mechi mbili, lakini yeye bado hajamaliza ligi hadi atakapopata pointi sita zilizobakia kwenye michezo hiyo mwili.
“Ligi haijaisha, suala la kupata ubingwa ni jambo moja, lakini kumaliza kwa ushindi ni suala jingine muhimu zaidi, naamini kuwa hilo ni jambo ambalo limebakia kwangu na benchi langu la ufundi kuhakikisha kuwa tunapata pointi sita kutoka kwenye mechi zetu zilizobaki," alisema.
Kutokana na hilo, kocha huyo aliingiza timu yake katika mazoezi ya gym, katika kituo cha mazoezi kilichopo jengo la Quality Centre kujiandaa na mechi hizo mbili dhidi ya Coastal Union na Simba.
Kwa upande wa baadhi ya wachezaji waliozungumza jijini, wameeleza furaha yao kutokana na matokeo hayo, lakini wakisema kuwa wanayo kazi ya kulipa kisasi cha mabao 5-0 za msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Mbuyu Twite, ambaye alidai ameupokea ubingwa huo kwa shangwe kubwa kwa sababu huu ni msimu wake wa kwanza na jambo zuri kumaliza ligi akiwa na medali ya ubingwa. Kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima, alisema jambo hilo linampa furaha kubwa na sasa anafikiria mpango wa kufanya mazungumzo ya kuweza kubaki kwenye kikosi hicho.
Yanga, ambayo kwa sasa imefikisha pointi 56 kwenye ligi baada ya kushuka dimbani mara 24, imebakiza mechi mbili dhidi ya Coastal Union itakayofanyika Mei Mosi na Simba itakayofanyika siku 18 baadaye, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...