Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 16, 2012

MATOKEO MABOVU OLMPIKI 2012 YAMKERA RAIS NIGERIA



LAGOS, Nigeria
 KUFUATIA Nigeria kuvurunda na kurudi bila hata medali moja ya mashindano ya Olimpiki 2012 jijini London, rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan ameagiza mageuzi na  mabadiliko makubwa na ya haraka katika tasnia ya michezo, kupitia wizara husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Nigeria, Labaran Maku, wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika Ikulu ya nchi hiyo, baada ya kikao cha kila wiki cha Rais na Baraza Kuu la Utendaji (FEC) Jumatano.
Waziri Maku alisisitiza kuwa, rais amesikitishwa kwa kilichofanywa na wawakilishi wa nchi hiyo jijini London, na kwamba ametaka kuwapo kwa haja ya kubadili mwenendo huo mbovu.
Kwa mujibu wa waziri Maku, rais Jonathan, ameagiza kuwapo kwa utaratibu wa wizara na vyama vya michezo kushirikisha serikali za majimbo, sekta binafsi na wadau wengine, ili kuweka kipaumbele cha mafanikio ya michezo nchini humo.
"Yeye (rais Jonathan) amesema kufanya kwetui vibaya jijini London, kuchukuliwe kama changamoto ya ya harakati mpya za kuirejeshea heshima michezo ya nchi hiyo ambayo, imeanza kupotea kutokana na lindi la kuvurundano kwenye mashindano makubwa.
"Rais Jonathan anaamini kwamba ili kubadili mazingira na hali ya sasa ya kufanya vibaya, tunahitaji wataalamu, tunahitaji mipango yakinifu na tunahitaji kufadhili michezo katika mfumo utakaowezesha nchi kurejesha mvuto na maendeleo katika sekta hiyo.
"Yeye anaamini kwamba katika mashindano yajayo ya Jumuiya ya Madola na Olimpiki ijayo ya mwaka 2016 nchini Brazil, lazima Nigeria kama taifa lilenge kutimiza malengo binafsi kayika ukuzaji wa michezo ili kuimarisha ushiriki wa wawakalishi," alisisitiza Waziri Maku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...