Mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti bw.Stephen Gannon (
kushoto ) akiongea na waandishi wa habari alipohudhuria kwa mara ya
kwanza droo ya mwishon ya promosheni ya Vumbua Hazina Chini ya Kizibo
iliyoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti tangu mwezi wa tano 2012
hadi leo. Kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni
hiyo Bi Teddy Mapunda.Mkurugenzi wa Masoko
wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw Ephraim Mafuru (kushoto) akiongea na
mmoja wa washindi katika droo hiyo ya mwisho kwa njia ya simu ya
kiganjani.(katikati) ni meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo na
kushoto ni wasimamizi na wakaguzi kutoka bodi ya taifa ya michezo ya
kubahatisha.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti kampuni ya bia ya Serengeti akiongea mna mmoja wa washindi katika droo ya mwisho ya Vumbua dhahabu Chini ya Kizibo iliyomalizika leo, kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo na katikati ni Tumainieli Malisa kutoka kampuni ya PWC
Hii ndiyo gari yenyewe aina ya Ford Figo iliyojipatia mshindi leo |
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti kampuni ya bia ya Serengeti akiongea mna mmoja wa washindi katika droo ya mwisho ya Vumbua dhahabu Chini ya Kizibo iliyomalizika leo, kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo na katikati ni Tumainieli Malisa kutoka kampuni ya PWC
Katika kipindi chote hicho, watanzania wengi wamekuwa wakifurahia kuwa watumiaji wakubwa wa bidhaa ama vinywaji vinavyozalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti hasa vinywaji vile vilivyoainishwa katika promosheni hiyo kutokana na kufululiza kutokea kwa washindi mbalimbali waliojishindia zawadi zikiwemo Gari mpya, bajaj, pikipiki jenereta pamoja pesa taslimu.
Asubuhi ya leo promosheni hiyo ilifika tamati katika ofisi za CMC Motors jijini Dar es Salaam ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa gari aina ya FORD FIGO lililopo kwenye promosheni hiyo ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ kwa kuchezesha droo ya mwisho kabisa.Droo hiyo kama ilivyo ada, ilipata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Awali akimkaribisha mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Steve Gannon anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Richard Wells na baadaye kuongea na waandishi wa habari katika mara baada ya kuchezesha droo hiyo ya mwisho mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru amesema zawadi nyingi zimekuwa zikienda kwa washindi wengi nchini kote.
Amewashukuru sana wateja na watanzania kwa ujumla kutokana na mwitikio na ushirikiano wao mzuri waliouonyesha katika kipindi chote cha promosheni hiyo. “Kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti nachukua fursa hii kuwashukuru sana tena sana wateja wetu na watanzania wote kwa ushirikiano wao mzuri waliotupa katika kipindi chote cha promosheni na kwamba tunatambua uwepo wao katika shughuli zetu zinazoendelea” alisema Mafuru huku akiongeza kuwa mwisho wa promosheni hii ni mwanzisho wa promosheni zingine nyingi.
Kwa upande wake mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon amesema amefurahishwa sana na jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi yake hasa inavyotekeleza sera zake za kuwa karibu na wateja wake bila kubagua, “Nimefurahishwa sana na jinsi kampeni hii maalum inayolenga kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla. Hata kama tumefikia mwisho wa kampeni hii, naomba watanzania wote wajue kwamba kuna promosheni nyingi sana za aina hii ambazo tutaendeleza na kuendelea kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla. ” alisema Gannon.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni ya “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’, nchi nzima kwa muda wa miezi kumi na Promosheni hiyo imeweza kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla
No comments:
Post a Comment