Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 15, 2012

SKYLIGHT BAND , MWASITI, SHILOLE KUNOGESHA IDD MOSI&PILI


 Kutoka kulia ni Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi akitoa wito kwa wadau wa muziki na wazazi kujitokeza siku hiyo ya onesho lao itakatofanyika Idd pili, anayefuata ni Aneth Kushaba mwanamuziki wa bendi ya Skylight.
 Hiki ndiyo kikosi cha bendi mpya ya Skylight wakionesha umahiri wao mbele ya wanahabari hawapo pichani.
BENDI ya muziki mpya inayokwenda kwa jina la Skylight  inayopiga muziki wake katika mtindo wa Afro Pop inatarajia kufanya maonesho yake  mawili ambayo yatafanyika Idd mosi na Idd pili  pia itakuwa ni sehemu ya kuizindua rasmi  bendi hiyo katika wigo mpana wa muziki wa dansi hapa  nchini.

Bendi hiyo iliyosheheni wanamuziki wenye uwezo na uzoefu  mkubwa hapa nchini  watatoa burudani katika sikukuu ya Idd pili katika hoteli ya Giraffe View iliyopo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Katika kunogesha uzinduzi huo Idd mosi  watasindikizwa na mwanamuziki Shilole na Idd pili watasindikizwa na Mwasiti Almasi.

Baadhi ya wanamuziki wanaounda bendi hiyo ni Jonico Flower aliyetamba tangu enzi za bendi ya Chuchu Sound,baadaye akatumikia bendi nyingine zenye majina makubwa, Sam Machozi, Sonny Masamba na Mary Lucas na wengineo.

Onesho hilo limepangwa kuanza milango ya saa tatu asubuhi kwa kiingilio cha sh. 5,000 na sh. 15,000 kwa wakubwa.

Baadhi ya nyimbo zao ambazo tayari wamerekodi ni pamoja na 'Wivu' ulipoigwa katika mahadhi ya Lingala,'Siku yangu' umepigwa katika mtindo wa Afro Pop, 'Yatakushinda' umepigwa katika mtindo wa miondoko ya ngoma ya pwani almaarufu 'Mduara'. zaidi tembeleahttp://bongoweekend.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...