Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 9, 2012

Mapacha Watatu ndani ya ‘Back in Town’ Mango





Na Elizabeth John

BENDI ya Mapacha Watatu ‘Wakali wa Town’, inatarajiwa kufanya onesho kubwa litakalojulokana kwa jina la ‘Back in Town’, litakalorindima ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, Oktoba 19 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Hamisi Dakota, alisema onesho hilo litakuwa la kwanza jijini, baada ya kuwa kwenye ziara ya Kampuni ya Vadocom, wakitangaza huduma ya M-Pesa mikoa mbalimbali.

“Tumerejea Dar es Salaam hivi karibuni, hivyo mashabiki wetu wasubirie kuona mambo makubwa katika onesho hilo, ambalo natumaini litakuwa la kukata na shoka,” alisema Dakota.

Dakota alisema, katika onesho hilo watasindikizwa na mwimbaji wa taarabu, Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’, ambako pia watatumia siku hiyo kuwatambulisha waimbaji, wapiga vyombo na wanenguaji wapya, ambao watajiunga na bendi hiyo.

“Hakuna asiyejua kazi yetu na wala hakuna asiyemjua Isha Mashauzi, mashabiki watarajie burudani safi kutoka kwetu,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...