Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 29, 2012

ARUSHA KUWA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI (ECAPBA).


 Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha  Mh. Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, EAC”Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
 Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
 Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa  ECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
 Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
 ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...