Dar es Salaam,Tanzania 18
Desemba, 2012. Tigo ina madhumuni ya kuweka tabasamu kwenye kila
uso wa mteja wake wa Tanzania, kupitia bidhaa na huduma zake bunifu na kwa
kuendelea kuwapa wateja wake kipaumbele kwenye mahitaji yao maalum, nchi nzima.
Kwa maana hii Tigo Tanzania,
mtandao wa bei nafuu , unaopatikana kote nchini kwa urahisi , unabadilisha slogan
yake kutoka “Express Yourself” kwenda ‘’Smile You’ve got Tigo” , yaani tabasamu
upo na Tigo.
Slogan
hii mpya inaonesha vile wateja wetu wanavyoridhika na aina mbali mbali ya
bidhaa zetu ambazo zipo sokoni, zinazoboresha maisha yao na kuwasaidia kwenye
shughuli zao za kila siku. Huduma kama Tigo Pesa zinazorahisisha utumaji na
upokeaji wa fedha nchi nzima.Tigo Telco Solutions maalum kwa wafanyabiashara, na hivi karibuni
Tigo imetoa vifaa vya nishati vya jua kwa kuchaji simu . Mradi
huu unatoa ufumbuzi kwa maeneo yasiyo na umeme, unasaidia ujasiriamali na
wakati huohuo unaokoa mazingira kwa kutumia nishati rafiki isiyoathiri
mazingira.
Programu kubwa ya Tigo ya
kurejesha kwa jamii ‘Reach for Change’ inasaidia wajasiriamali wa miradi ya
kijamii na itawagusa watoto na vijana wengi wa kiTanzania.
‘’Hizi programu,bidhaa na
huduma, na nimegusia chache tuu, bila shaka zimeweka tabasamu kwenye nyuso za
wateja wetu. Pia kupewa nafasi ya juu kimataifa, kwenye huduma kwa wateja
kupitia mtandao wetu, inaoyesha kwamba juhudi zetu zinaonekana na
zinakubalika.” Alisema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
Tigo inataka kuwapa wateja njia ya kujieleza na zaidi .
‘’Tigo Tanzania inalenga kuwapa wateja wake
bidhaa, huduma bora , na mtandao wa uhakika. mbali mbali, mtandao na huduma kwa
wateja bora .Kibiashara Tupo kwenye familia ambayo inatoa huduma kwa zaidi ya
watu milioni 43 dunia nzima , na tunataka wateja wetu wawe na raha na
kutabasamu kwasababu wana mtandao wa Tigo” alisema Bwana Gutierrez.
Kuhusu Tigo
Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi
Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na Zanzibar. Tigo
imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma zake za simu nchini
Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye
kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa
huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi
kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na
Amerika ya Kusini.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
I'm curious to find out what blog system you have been using? I'm experienсing somе small security іѕsuеѕ ωіth mу lateѕt wеbsite and
ReplyDeleteI ωould lіkе to fіnԁ sοmething mоre secuгe.
Dο уou haѵe anу recommenԁations?
Αlsο vіsіt my web blog natural breast augmentation