Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia)
akimkabidhi mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki mkoa wa
Mwanza Makoye Bunoro Shilingi 50,000/= kwa ajili ya kuweka mafuta katika
pikipiki za kitengo cha Polisi jamii pale wanapoenda kupambana na
wahalifu.Umoja huo unawasaidia waendesha pikipiki 2034 kupata leseni
na mafunzo yaliyotolewa na Chuo cha VETA kwa gharama naafuu.
Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia)
akiongea jambo hivi karibuni na viongozi chama cha Umoja wa wapanda
pikipiki wa mkoa wa Mwanza (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao
eneo la Mlango mmoja ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Mdhibiti
wa mali za chama cha Umoja wa wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza
Faraji Abdalah (kushoto) akimwelezea Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara
ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) jinsi umoja huo
ulivyoweza kuunda kitengo cha polisi jamii ambacho kinashirikiana na
Jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni Mwenyekiti wa
Umoja huo Makoye Bunoro.
Viongozi
wa Umoja wa wapanda Pikipiki wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James
Kajugusi (hayupo pichani) akiwaeleza jinsi wanavyoweza kuunda SACCOS
yao na kukopa fedha kutoka mfuko wa vijana ambazo zitawasaidia kununua
pikipiki zao na kujiajiri wakati alipowatembelea ofisini kwao ili kuona
shughuli zinazofanywa na umoja huo.
No comments:
Post a Comment